Habari za Punde

Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wanawake wa Mother Cycle. Watowa Mafanikio Kwa Wanawake wa Shehia za Zanzibar.

Mratibu wa Mradi wa Mother Cycle Bi. Aisha Ali Karume akitowa maelezo wa Mradi huo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Wanawake wa Nyumbani, na kukabidhiwa Vyeti na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar Bi. Nasma Chum, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya ZAYEDESA Mazizini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Women Without Border ya Austria (WWB) Dr.Edit Schlaffer, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Vyeti kwa washiriki wa mafunzo hayo yaliowashirikisha Kinamama kutoka Sheria mbalimbali za Unguja na kusema Wanawake ni walimu wazuri kwenye familia kwanu hufanya maamuzi yao mazuri katika familia yake, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya ZAYEDESA mazizini Zanzibar. 

Katibu wa Taasisi ya ZAYEDESA Zanzibar Bi. Lucy Majaliwa akizungumza wakati wa hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo ya Wanawake kuwajengea uwezo katika familia na jamii iliotolewa kupitia Mradi wa Mother Cycle, na kuwashirikisha Wanawake 60 kutoka shehia za Unguja.
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar, Bi. Nasima Chum, akitowa nasaha zake wakati wa kuyafunga mafunzo huo ya Wanawake kuwajengea Uwezo katika familia na jamii wanapokuwa majumbani, yaliotolewa na kupitia Mradi wa Mather Cycle chini ya Jumuiya ya ZAYEDESA kwa kushirikiana na WWB, ya Nchini Austria.








No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.