Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Aendelea na Ziara Yake Kisiwani Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akianza  ziara ya siku Tatu Kisiwani Opemba kukagua Miradi ya Maenddeleo pamoja na kuangalia changamoto zinazowakabili wa Wananchi.Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Kuisi Pemba Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdullah.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano ya Usafirishaji Zanzibar Nd. Shomar  Omar Shomar Kulia akimueleza Balozi Seif  hatua zilizochukuliwa za ujenzi wa Bara bara ya Kijiji cha Ngomeni Mkoa Kusini Pemba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwanasihi Wananchi wa Kijiji cha Ngomeni kuendelea kuitunza Bara bara yao ili iwe na uwezo wa kudumu kwa kipindi kirefu zaidi.
Daktari Dhamana wa Wailaya ya Mkoani Pemba Dr. Mohamed Ali Jape Kushoto akifafanua jambo mbele ya Balozi Seif  aliyefika katika Kijiji cha Ngomeni Mkoa wa Kusini Pemba kukagua Maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kijiji hicho.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddia alisema kwamba maendeleo makubwa hupatikana mahali popote pale iwapo mawasiliano ya Bara bara yatajengewa  miundombinu  imara  na ya kudumu.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuzitia Lami Bara bara zote zilizojengwa kupitia Mradi wa MIVA katika hatua ya kifusi ili kuimarisha Sekta hiyo ya Mawasiliano ambayo ndio msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akianza ziara ya Siku Tatu Kisiwani Pemba kuangalia Miradi ya Maendeleo pamoja na kufuatilia changamoto zinazowakabili Wananchi pamoja na Taasisi za Umma ambapo alipata fursa ya kuikagua Bara bara ya Kijiji cha Ngomeni yenye urefu wa Kilomita 3.3.
Alisema ujenzi wa Bara bara za Vijijini zilizojengwa kupitia Mradi wa MIVA ulilenga kuwaondoshea shida za usafiri Wananchi wa Vijijini wawe na uwezo kamili wa kupata usafiri wa uhakjika sambamba  na kusafirisha  mazao yao kupelekea sokoni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alinawasihi Wananchi watakaoitumia Bara bara hiyo ya Ngomeni kuwa waangalifu katika matumizi yake ili iweze kudumu kwa muda mrefu kwani imejengwa kwa nia ya kuwaondoshea ufumbufu wao.
Mapema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Nd. Shomar  Omar alisema ujenzi wa Bara bara  uliofanywa  kwa hatua ya kuwekwa Kifusi katika hatua za Awamu ya kwanza ulianza mnamo Mwaka 2014.
Nd. Shomari alisema Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana na Mfuko wa Bara bara Zanzibar zimeanza mpango wa kuzitia Lami Bara bara zote zilizojengwa kupitia Mradi wa MIVA  kuitikia Agizo la Rais wa Zanzibar la kuzitaka  Bara bara zote za Vijijini zilizojengwa kupitia Mradi huo kuwekwa Lami .
Naibu Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Ujenzi alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba kazi iliyobakia kwa sasa ni ujenzi wa Mkitaro pembezoni mwa Bara bara hiyo licha ya changamoto iliyopo ya wembamba wa Bara bara hiyo kutokana na maumbile yake.
Alieleza kwamba ujenzi wa Bara bara hiyo umegharamiwa kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Mfuko wa Bara bara  kwa kiasi cha shilingi Milioni 588,000,000/-.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikagua maendeleo ya Ujenzi wa Kituocha cha Afya cha Kijiji cha Ngomeni kiliopo Jirani na Bara  bra hiyo.
Daktari dhamana wa Wilaya ya Mkoani Pemba Dr. Mohamed Ali Jape alisema kukamilika  kwa Kituo hicho kilichoanza kujengwa Mwaka Mmoja uliopita kitaweza kuwaondoshea shinda Wananchi wa eneo hilo ya kufuata masafa marefu  huduma za Afya.
Dr. Jabir alisema zaidi ya Wananchi Mia Tatu wanaweza kupata huduma za Afya kwenye Kituoni hicho kinachotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi Milioni Mia 106 ambapo gharama kamili hadi kumalizika kwake zinatarajiwa kufikia Shilingi Milioni 197,000,000/-.
Naye Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Kisiwani Pemba Bibi Shadya Shaaban alimueleza Balozi Seif kwamba wapo vijana wa Kijijini ambao tayuari wameshapata mafunzo ya Afya lakini mchakato wa kufanyiwa ajira bado haujafanyika hadi sasa.
Alisema Vijana hao waliamua kupata mafunzo hayo na kuacha kutegemea Vijana wa Maeneo mengine ambao wakati mwengine hawaaminiki ili kusaidia kuwaondoshea shinda Wawazi wao pamoja na Ndugu na Jamaa zao.
Akitoa shukrani zake kwa hatua kubwa ya ujenzi wa Kituo hicho cha Afya cha Kijiji cha Ngomeni Makamu wa Pili wa Rais wa anzibafr Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali Kuu itajitahidi kuweka Dawa na Vifaa Kituoni hapo ili kitoe huduma za Afya kama kilivyokusudiwa.
Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefikia maamuzi ya kuiongezea fedha za kutosha Wizara ya Afya Zanzibar  kwa lengo la kukamilisha mipango za Sera za Afya za kuwapatia huduma Wananchi walio wengi bila ya usumbufu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.