Habari za Punde

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale ziarani kisiwani Pemba kujitambulisha

 WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, mhe:Mahmoud Thabit Kombo akisalimiana na Mwakilishi wa jimbo la Ziwani Suleiman Makame, mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba kwa lengo la kujitambulisha kwake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mhe:Mahmoud Thabit Kombo, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla,alipofika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha kwake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 OFISA Mdhamini Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Pemba, Khatib Juma Mjaja akiutambulisha ugenzi wa Wizara hiyo, wakiongozwa na waziri Mahmoud Thabit Kombo, wakati walipofika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, kwa lengo la kujitambulisha kwao.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla akizungumza na ujumbe wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, ulipofika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha kwao.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe:Mahmoud Thabit Kombo, akizungumza katika kikao cha pamoja na Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla wakati alipofika kujitambulisha kwake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)
 WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo akiangalia moja ya mashine zilizomo katika chumba ya IT katika jengo la Taasisi za nyaraka na Kumbukumbu Pemba, wakati wa ziara yake ya siku mbili Kisiwani Hapa.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo, akieleza jambo wakati alipokuwa akiangalia kumbukumbu katika jengo la Makumbusho ya mambo yake Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.