Agizia kikapu chako cha Ramadhaan kusaidia ndugu zetu Zanzibar, Tanzania
Assalaamu Alaykum WarahmatuLlaahi Wabarakaatuh
Mwezi mtukufu wa Ramadhaan umekaribia.
Jumuiya ya Al Iman ya Northamptonshire nchini Uingereza ni Jumuiya ya Waislamu wanaozungumza kiswahili imeamua kuendeleza “Kikapu cha Ramadhaan” (Ramadhaan Basket) kama tulivyoweza kufanikisha mwaka jana Bi idhni Llaah
Kwa Pauni £15.00 tu unaweza kujipatia kikapu chako na mchango wako kama ni sadaka yako kwa ndugu zetu katika mwezi mtukufu wa Ramadhaan.
Tunakuomba kwa moyo mkunjufu, andaa kikapu chako sasa na Allaah ‘Azza wa Jall atakulipa kwa mchango wako kwa kuchangia Pauni 15.00 tu kwa kikapu kimoja. (unaweza kuongeza vikapu zaidi ukihitajia)
Kwa mwaka huu kikapu chetu kitakuwa na:
Mchele 10kg
Unga ngano 5kg
Sukari 2kg
Maharagwe 2kg
Unga wa sembe 2kg
Mafuta ya kupikia 2lt.
Kikapu hichi kitakugharimu Pauni 15 tu kukinunua na kukigawa.
Kutuma mchango wako online Transfer, Lloyds Bank, Sort Code 309609 Account 03539228
Tumia reference: ‘Ramadhaan Basket’
Kama utachangia kwa njia ya cheki hakikisha cheki imeandikwa na kulipwa kwa Al – Iman Society of Northamptonshire
Na upande wa nyuma iandikwe: ‘Ramadhaan basket’
Au unaweza kutuletea kwenye Msikiti wetu: Northampton Mosque & Islamic Centre, Clare Street, Northampton NN1 3JF
Kwa maelezo Zaidi na ufafanuzi wasiliana na Amiyr wa Jumuiya: Ustaadh Abdulrazak +44 7951816208 au email iman@al-iman.co.uk
Al Iman Society of Northamptonshire ni Jumuiya iliyosajiliwa kama Jumuiya ya khiari yenye makaazi yake Northampton UK ikiwa na namba ya usajili 1117020
Baaraka Llaahu fiykum
No comments:
Post a Comment