Habari za Punde

Best of Zanzibar yajenga vibaraza vya kusomea Chuo cha Utumishi wa Umma IPA



Katika kuendeleza elimu na kuchangia kwenye jamii Best of Zanzibar imejenga vibaraza vya kusomea vilivyo gharimu Tsh 4,300,000/-, katika Chuo cha Utumishi wa Umma (IPA) kilichopo Tunguu.

Hii ni moja katiya kutekeleza malengo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwenye kukuza elimu ya juu.

Best of Zanzibar inashirikiana sambamba na serekali ya Zanzibar kwenye kuhakikisha tunaleta maendeleo na kuboresha elimu katika nyanja mbali mbali.

Uzinduzi wa vibaraza hivyo ulifanyika katika hafla ndogo chuoni hapo, na Balozi Amina Ali Salum Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko akiwa Mgeni rasmi katika sherehe hiyo.

“Tunawashukuru sana Pennyroyal kwa kujitolea kujenga sehemu za kukalia wanafunzi. Pennyroyal ni miongoni mwa wawekezaji hapa Zanzibar waliyo jikita kwenye maswala ya kijamii na kua mfano mzuri wakuigwa.”

Mkurungenzi Mkuu wa kampuni ya Pennyroyal Ltd Bw. Brian Thomson alikua na haya yakusema, “Chuo cha IPA ni miongoni mwa chuo vinanyo onesha maendeleo makubwa kwenye sekta ya elimu Zanzibar. Pennyroyal na mradi wake wa kusaidia jamii Best of Zanzibar, inawaunga mkono na kuwasaidia kuyaendeleza maendeleo hayo. 

Best of Zanzibar ina malengo ya kueneza huduma zake kwenye maeneo mbali mbali hapa Zanzibar. Ikiwemo na kumejenga vituo vya polisi Jambiani na Kiboje ili kuimarisha ulinzi kwenye maeneo hayo. Vile vile tumejenga kituo cha watu wenye ulemavu jimbo la Shaurimoyo.

Chuo hicho kina wanafunzi 1287 na kutoa masomo mbali mbali yakiwemo Masomo ya Kimataifa na Displomasia, Record Management, Secretary course, Economy and Finance, Information Technology na Local Management.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.