Habari za Punde

Mashindano ya 26 ya Kimataifa ya Afrika Mashari ya Kuhifadhisha Qur-An Juzuu 30 Hifdhi na Tashjee Yalioanfdaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-An Zanzibar Yalioandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur-An Zanzibar Yaliofanyika Katika Masijid Jaamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar.

Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam ya Kuhifadhisha Qur-An Zanzibar Sheikh Suleiman Omar Ahmad (Mwalimu Sule) akizungumza na kutowa historia ya jumuiya hiyo tangu kuazishwa kwake miaka 26 na hatua iliofikia hadi sasa katika kuendelea na kuinua vipaji vya Wanafunzi katika kuhifadhi Qur-An Juzuu 30 kwa njia za Hifdhi na Tashjee. kwa sasa wanafkia kiasi cha Wanafunzi zaidi ya 500 Zanzibar.
Mfanyabiashara maarufu Zanzibar Said Nassor Seif (Bopar) akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Waumini na Wafanya Biashara Zanzibar kujitokea katika kusaidia shughuli za kijamii na kukuza vipaji vya Watoto wetu katika kuinua uwezo wao wa kuhifadhi Qur-An hapa Zanzibar na kuahidi kuisaidia Jumuiya hiyo Computer 15 ilikuboresha maandalizi ya mashindano mbalimbali ya kuhifadhisha Qur-An Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar kutumia muda wao katika kipindi hicho cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kutekeleza Ibada ya kuutumia kwa kusoma Qur-an kuacha kutumia muda wao kwa michezo ya karata, bao na keram.



















No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.