Habari za Punde

Katibu Mkuu wa Mambo ya Kale wa Oman Mr. Salim Mohammed Amaliza Ziara Yake Zanzibar na Kutembelea Jumba la Beit Al Jaib Zanzibar, Ambalo Litafanyiwa Matengenezo Makubwa na Serikali ya Oman.

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi zawadi ya picha inayoonesha mandhari ya eneo la bustani ya forodhani Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Kale wa Oman Mhe. Salim Mohammed Al Mahrouk, baada ya kumaliza ziara yake ya Kiserikali Nchini Zanzibar na kupata fursa ya kutembea maeneo mbalimbali ya Historia ya Zanzibar.
JENGO la kihistoria la Beit el ajab liliopo Forodhani Mjini Zanzibar linalotarajiwa kufanyiwa matengenezo makubwa na Serekali ya Oman baada ya kubomoka baadhi ya sehemu zake miaka michache iliyopita.
WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza katika hafla ya kumuaga  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Oman Salim Mohammed Almaharouk ( kushoto) iliyofanyika katika jengo la kihistoria la Beit el ajab Forodhani. Wa kwanza (kulia)  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Dkt. Amina  Ameir  na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Khadija Bakari Ali.
KATIBU MKUU Wizara ya Mambo ya Kale wa Oman Salim Mohammed Almaharouk akizungumza na Viongozi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar kuhusu matengenezo makubwa ya Jengo la Beit el ajab ambalo lilibomoka miaka michache iliyopita, (kulia)  Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mahmoud Thabit Kombo.
WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akimkabidhi zawadi mbalimbali Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Oman Salim Mohammed Almaharouk baada ya kumaliza ziara ya kutembelea Maeneo mbalimbali ya historia ya Zanzibar.
WAZIRI wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akiagana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Kale wa Oman Salim Mohammed Almaharouk baada ya kumaliza ziara yake Zanzibar.
(Picha na Abdalla Omar Maelzo Zanzibar).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.