Habari za Punde

Wananchi wa Zanzibar Wakiwa Katika Harakati za Maandalizi ya Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani Unaotarajiwa Kuaza Kesho Mfungo Huo.Wakiwa Katika Marikiti Kuu ya Darajani Unguja.

Wananchi wa Zanzibar wakiwa katika harakati za maandalizi ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuaza kesho kufuatilia muandamo mwa mwezi leo.
Bei za bidhaa za matunda ya aina mbalimbali hutumika sana katika kipindi hicho zikiwa zemejaa katika Marikiti Kuu ya Darajani, katika marikiti hiyo kumekuwa na wingi wa bidhaa hizo na bei zake kiasi za kuridhisha, chana moja ya ndizi aina ya mtwike inauzwa kuazia shs.3000/= inategemea ukubwa wake, boga limeaza kwa bei ya shs.2500/= kutegemea ukubwa wake fungu la majimbi limeuzwa shs 5000/= na shs 2000/=  na Viaza vitamu fungo moja limeuzwa shs.5000/= na 2000/= katika Marikiti hiyo 
Kilo moja ya Tungule inauzwa shs. 3000/= kwa kili moja na vitunguu maji kilimo moja shs 3500/= mbatata kilo moja inauzwa shs 1000/=  jioni ya leo katika marikiti hiyi kuu ya darajani Mjini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.