WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya
China Cilil Engineering Construction Corporation, walip inayoteIIVIL
ofika Ofisini kwake kwa kukabidhi Vyakula kwa ajili ya kuwasaidia Wananchi
waliopata maafa ya Mvua katika sehemu mbalimbali za Unguja, hafla hiyo
imefanyika katika ukumbi wa Ofisi yake Vuga Zanzibar
MWAKILISHI wa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation
David Yan, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi msaada kwa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud,
walipofika kukabidhi msaada huo wa Vyakula, hafla hiyo imefanyika katika Ofisi
ya Makamu Vuga Zanzibar
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed
Aboud Mohammed, akipokea mafuta ya kula kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya
Ujenzi ya China Civil Engineering Construction Corporation, inayotengeneza
barabara ya Bububu hadi Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa ajili ya
Wananchi waliopata maafa ya mvua za masika Unguja, walikabidhi vyakula Mchele,
Sukari na Unga wa ngano.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed
Aboud Mohammed akitowa shukrani kwa msaada huo wa vyakula baada ya kukabidhiwa.
na Mwakilishi wa Kampuni ya Ujenzi wa Barabara ya China CIVIL Mr. David
Yan,hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Vuga Zanzibar.
No comments:
Post a Comment