Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi leo

Na Ali Issa na Bahati Habibu Maelezo Zanzibar 22/5/2018
Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilitoa tahadhari ya kuhama wananchi wanao ishi sehemu hatarishi kufuatia mvua zinazo endelea kunyesha kila uchao kabla ya kuja mvua hizo na kuathiri hivi sasa.
Hayo yamesemwa leo huko Baraza wa wakilishi nje kidogo ya mji wa Zanzibar na naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mihayo Juma Nunga wakati akijibu Sali la mjumbe Jaku Hshimu Ayoub aliotaka kujuwa kua Serikali imejipanga vipi kukabiliana na maafa ya mvua zinazo endelea kunyesha na kuna fedha na rasilimali za kutosha na mvua hizo.
Amsema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imaejipanga vyema kukabiliana na maafa  yatokanayo na mvua zinazo endelea kunyesha kwa kuchukuwa hatua mbali mbali ikiwemo kutoa tahadhari kupitia vyombo vya habari kwamba kutakuwa na mvua kubwa na wananchi walitakiwa kuhama kabla ya mvua hiyo kuja.
Amesema hali hiyo huwa haitarajiwi kuwa itakuwa ya kiasi gani kwani ni jambo la dharura lakini hata hivyo serikali yake imejipanga vyema kuhakisha wanakabiliana nalo.
“suala la maafa ni jambo la dharura ambalo halipimiki na maranyingi hutokea ghafla bila kutarajia ,lakini erikali kama ilivyo desturi yake imejipanga kukabiliana na maafa kwa kadiri itakavyo wezekana,”alisema Naibu Waziri.
Wakati huohuo waziri huyo aliendelea kumjibu Jaku Hshimu Ayoub  aliotaka kuona kuwa wananchi wa zanibar wategemee nini kwa kundwa wizara moja mpya.
Waziri huyo alisema kuwa madhumuni na malengo makubwa ya ya serikali kufanya mabadiliko  hayo ni kutimiza azma ya kuwatumikia wananchi wao  ikiwa nifrusa ya kikatiba chini ya ibara ya 53(a) ya katiba ya zanzibar ya mwaka 1984.
Aidha alisema kuwa ni utaratibu wa kawaida wa serikali zote duniani kwa mazingira na uwajibikaji mzuri zaidi wa serikali kwa wananchi wake.
Hata hivyo alisema kuwa undwaji wa wizara hiyo ni kurahisisha upatikanji wa huduma bora kwa wananchi na utendaji mzuri wa serikali .
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya kale Mahamud Thabiti Kombo amesema kuwa serikali imeangalia umuhimu wa kuwajiri wakalimani wa lunga za alama kupitia shirika la utangazaji la zanzbar ZBC ikiwa ni frusa ya kupata matangazo walemavu viziwi na watu wenye mahitaji kama hayo.
Hayo ameyasema leo huko baraza la wakilishi nje kidogo ya mji wa Zanzibar wakati akitoa majumuisho ya wajumbe walio uliza masuala yao na kuona kuwa ipo haja sasa ZBC kuwa na wakalimani wa lugha za alama wakati wakiendesha vipindi vyao  mbalimbali.
Amsema wataalamu hao wataajiriwa kupitia zbc na kuonana kwaza na mkuruzugenzi mkuu wa shirika hilo Aimani Duwe.
Amsema bila kiziwizi ajira hiyo ipo ili wale viziwi nao wafaidike kupokea matangazo yanayo endeshwa na ZBC.
AIDHA alisema kuwa  wandishi wa habari wanao jitolea katika vyombo vya habari vya serikali ambao wana muda wamiaka mitano na kuendelea nawao kunahaja nao kupatiwa ajira hiyo wakiwa wanafanya kazi muda wote katika tasisi zao.
Alisema ajira hiyo ni kwa wale wanao tumikia vyombo hivyo na sio wale wanao uza habari nje ya vyombo vyengine  wanao jitegemea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.