Habari za Punde

MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA BUBUBU HADI MKOKOTONI KUANZA JUNE 10 MWAKA HUU

Na Khadija Khamis –Maelezo 30/05/2018.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano  na Usafirishaji Dkt Sira  Ubwa Mwamboya amewataka wakandarasi wa ujenzi wa barabara  kutoka Bububu hadi Mkokotoni kuwa makini katika kuhakikisha ujenzi unafanikichwa kwa kiwango bora na cha uhakika .
Aliyasema hayo huko katika kijiji cha pale kiongoni Mkoa Kaskazini A wakati alipofanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali  ambayo yanatarajiwa kufanyika ujenzi huko  .
Alisema lengo kuu la Serikali ya Mapinduzi  ya Zanzibar ni kuhakikisha wananchi wake wanajipatia maendeleo ya kiuchumi kijamii na kiutamaduni hivyo  kuwataka wakandarasi hao  kujenga barabara kwa kiwango  bora na ufanisi mkubwa ili  kufikia asma ya serikali ya kukuza uchumi na kupunguza umasikini
 Aidha alisema Mradi huo wa Ujenzi wa Miundombinu hiyo itazihusisha barabara ya Bububu Mahonda Nungwi hadi Mkokotoni  inakadiriwa kufikia kilomita 52 ambayo inatarajiwa kuanza  kazi june 10 ,2018 hadi kufikia 2020 inategemewa kuchukua zaidi ya miezi 18 hadi kumalizika kwake .
Nae Mkurugenzi Mipango Sera Utafiti wa Mawasiliano na Usafirishaji Khatib Mohamed Khatib amesema mradi huo wa ujenzi  umefadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya afrika (ADB) ambao umegharimu  zaidi ya shilingi bilioni 58 .
Alifahamisha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itasaidia kulipia fidia zote za maeneo ambayo yatayoadhirika na ujenzi huo pamoja na fidia za wakulima wataovurugiwa konde zao katika maeneo yote yatayofika ujenzi huo
Mkurugenzi huyo alisema kampuni ambayo imefanikiwa kupewa mradi huo wa ujenzi  kutoka Bububu hadi Mkokotoni  ni kampuni ya kichina iitwayo M/S  China civil engineering construction corporation (CCECC)
Aidha alisema katika ujenzi huo unatarajiwa kujengwa barabara ya Pale Kiongele hadi mkokotoni ambao eneo hilo litachukuwa zaidi ya kilomita 4,61pamoja na madaraja mawili ambayo yanatarajiwa kuwa na ubana 10.5 .
Hata hivyo alisema ujenzi huo unaotarajiwa kuanza hivi karibuni kuanzia Bububu Mahonda hadi Mkokotoni ni sawa na kilomita 31,  Fuoni hadi  kombeni kilomita 8.58.pamoja na Pale Kiongele kilomita 4.61  na Matemwe hadi Muyuni kilomita 7.580 .
Alisema kampuni hiyo  ya CCECC ilitiliana saini na Serikali  ya Mapinduzi Zanzibar  tokea juni 11 mwaka uliopita na kutarajiwa kuanza kazi oktoba 2017 kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa kuwepo kwa mvua kubwa kampuni ilishindwa kuanza kazi na inatarajiwa kuanza ifikapo juni kumi mwaka huu.
Nao Mkandarasi wa kampuni hiyo wamesema watahakikisha ujenzi huo utakuwa botra na wakiwango hata ikiwepo changamoto ambazo zitajitokeza katika harakati wa ujenzi huo watajitahidi kukabiliana nazo ipasavyo ili malengo yaliyokusudiwa yafikiwe.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.