Habari za Punde

Vyombo vya habari vya serikali vyatakiwa kulipa Mirabaha kwa wasanii

Ali issa na Bahati Mahamoud Maelezo 
Vyombo vya habari vya Serikali vimetakiwa kuharakisha kulipa deni la mirabaha million 80 zinadaiwa kuwalipa  wasanii ambao hawajapata    stahiki zao zinazotokana na kazi zao kutumika na vyombo hivyo kwa muda mrefu.
Hayo yameelezwa leo  huko baraza la wakilishi nje kidogo ya mji wa Zanzibar  na Wanu Hafidhi Ameir mwakilishi wa viti maalum wanawake kutoka Kusini Unguja wakati alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya makadirio ya wizara ya vijana utamaduni na michezo huko Chukwani.
Amsema  shirika la ZBC ndilo ambalo linaongoza kutokulipa mirabaha ya wasanii tokea lilipolipa mwaka 2014 hadi sasa bado hawajalipa  jambo linarejesha nyuma maendeleo ya wasanii kutokana na kazi kutumika bila ya wao kupata stahiki zao kupitia kazi zao.
“Kazi za wasaninii zinatumika lakini wao wenyewe hawalipwi huku ni kurudisha juhudi zao za utendaji”alisema mwakilishi huyo.
 Aidha mwakilishi huyo alisema deni hilo lilipwe iliwasanii hao wafaidike na kazi zao.
Hata hivyo mwakilishi huyo aliongeza kwa kusema kuwa ukiacha vyombo vya serikali pia kuna vymbo vya binafsi vinadaiwa kulipa kazi za wasanii kitu ambacho haifai kuwafanyia wasanii.
Akitaja baadhi ya vyombo hivyo ni pamoja   tasisi ya Zanzibar Cable na vyenginevyo. 
Wakati huo huo mheshimiwa Hidaya Makame ameishauri taasisi inayoshughulikia michezo kuwatumi vijana wanaotoka maeneo ya shamba kushiriki katika vilabu vinvyoshiriki michezo ya kitaifa na mataifa ili kuendeleza vipaji vyao.
Alisema mjini wapo vijana wenye vipaji kimichezo lakini pia na  mashamba kuna vijana wenye vipaji hivyo watumike na wao kushiriki katika michezo.  
Aidha alisema  serikali itumie ngoma zake za asili wakati wa sherehe zao ikiwa ni njia mojawapo  kutangaza asili yao kupitia sanaa.
Nae muheshmiwa Sarahan mwakiliishi wa jimbo la ameishauri serikali  kuundaa mashindano yatakayowashirikisha wanafunzi wa skuli tofauti ili kuibua vipaji ambavyo vikiedelezwa itawasaidia vijana hao kujiajiri wenyewe

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.