Habari za Punde

Yaliojiri Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jijini Dar es Salaam Leo..

Mwenyekiti wa CCM Taifa pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt.John Pombe  Magufuli (kulia)  alipokuwa akiteta jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Taifa Mzee Abdulrahman Omar Kinana alipokuwa akiwashukuru wajumbe katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) mara baada ya kukubaliwa kustaafu baada ya kutumika nafasi hiyo kwa muda mrefu,wakati wa Mkutano   uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wajumbe walipokuwa wakisoma Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) uliofanyika leo chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe  Magufuli (hayupo pichani)    katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Jijini Dar es Salaam,
 Mwenyekiti wa CCM Taifa pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt.John Pombe  Magufuli (kushoto)  alipokuwa akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Taifa Mzee Abdulrahman Omar Kinana  baada ya kumalizika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Jijini Dar es Salaam, 
Mwenyekiti wa CCM Taifa pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt.John Pombe  Magufuli (kushoto pichani)  alipokuwa akipeana mkono wa pongezi na Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Taifa Mzee Abdulrahman Omar Kinana mara baada ya kukubaliwa kustaafu katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(NEC) uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano Ikulu Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.