Habari za Punde

Benki ya NBC yaandaa futari kwa wateja wake Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Ndg. Theobald Sabi  alipowasili katika viwanja vya hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar kuhughuria hafla ya Iftar ilioandaliwa na NBC kwa Wateja wao wa Zanzibar.i 


Rais wa Zanzibar  wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein ameipongeza benki ya taifa ya biashara NBC kutokana na kasi yake na juhudi za kukuza uchumi wa Zanzibar.

Akizungumza kwa niaba ya rais wa Zanzibar katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo ya NBC iliyofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Zanzibar Mkuu wa mkoa wa mjini Magharib Ayoub Mohammed Mahmoud amesema pato la taifa limekuwa likikuwa mwaka hadi mwaka kutokana na mchango unaotolewa na taasisi mbali mbali ikiwemo benki ya NBC.

Aidha Dk.Shein ameihimiza benki hiyo kuendelea na juhudi zake za kuimarisha mazingira bora na huduma kwa wateja wake ili kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko ya huduma za kifedha yanayotokea siku hadi siku na kukuza maendeleo bora nchini.

Dk Shein meipongeza Benki hiyo kwa kuonesha umuhimu kwa wateja wake kwa kurejesha miongoni mwa faida wanazozipata ikiwemo kwa njia hiyo ya kufutarisha na kutoa huduma nyengine mbali mbali kwa jamii.

Awali akizungumza katika hafla hiyo ya Futari kaimu mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Benki ya NBC Dk.Kassim Hussein amesema kukuwa kwa huduma za kuifedha Zanzibar pia kunatokana na huduma bora zinazotolewa na benki hiyo inayokwenda sambamba na mahitaji ya wateja wake.

Amesema mazingira salama yaliopo Zanzibar yanayoimarishwa na viongozi wakuu wan chi imewezasha Benki hiyo kufanya kazi zake za kutoa huduma za kifedha kwa ufanisi na umakini zaidi.

Dk.Kassim amesema  licha ya huduma mbali mbali zinazotolewa na benki hiyo pia ameanzisha huduma za kibenki ya kiislam ambayo inatoa huduma za mikopo kwa misingi ya sharia ya kiislamu .

Hivyo ametoa wito kwa wananchi kutumia benki hiyo katika kufanya miamala mbali mbali bila kujali misingi ya dini kwani ni salama katika ukuwaji wa uchumi nchini.

Katika Hafla hiyo ya futari iliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein , mawaziri , Jaji mkuu , Mufti mkuu wa Zanzibar na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wateja wa benki ya NBC .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.