Habari za Punde

Jeshi la Polisi Kisiwani Pemba Lakamata Dawa za Kulevya.


Na.Salmin Juma.- Pemba.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Jeshi la Polisi Kisiwani Pemba lafanikiwa kukamata dawa za kulevya  katika zoezi linaloendelea, Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamanda ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba RPC Shehan Mohd Shehan.

Tokea tarehe 20 / 05 /2018 Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba lilianza kuendesha operesheni maalum ya kupambana na uhalifu pamoja na madawa ya kulevya.
Miongoni mwa matukio yaliyopatikana ni yafuatayo.

06/06 /2018 saa 9 jioni huko Minazini Chakechake, jeshi la polisi lilimkamata Husein Suleiman Hassan (20) akiwa na unga unaodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya ambao alikua ameufunga katika makaratasi ya gazeti, kwasasa mtuhumiwa yupo chini ya uwangalizi wa jeshi hilo na hatua nyengine za kisheria zinafuata.

11/06/2018 mchana , hukohuko minazini chakechake , Jeshi lilimkamata Najim Ali Omar (54) mkaazi wa misufini , alipatikana na pombe ya kienyeji aina ya gongo nyumbani kwake,katika kidumu cha lita 10 ,mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi na anaendelea kuhojiwa ili kufikishwa mahakamani.

13/06/2018 saa 11:30 jioni huko Ole kianga,Yassir Nassor Hamadi (20) mkaazi wa Ole kianga alikamatwa akiwa na majani makavu yanayosadikiwa kuwa ni bangi (nyongo 8) akiwa ameyahifadhi ndani ya suruali,mtuhumiwa yupo chini ya uwangalizi wa jeshi la polisi , hatua za kumuhoji zinaendelea.

15/06/2018, saa 2 usiku, chakechake mjini , Hassan Bakari Hassan (37) mkaazi wa misufini chakechake amekamatwa akiwa na mirungi ndani Ya mfuko mwekundu, furushi moja lililojaa, mtuhumiwa yupo chini ya jeshi la polisi kuhojiwa kisha kufikishwa mahakamani.

16/06/2018 ,saa 9:30 jioni huko pujini dodo, Jeshi la polisi limemkamata Jizahibu Ali Amour (24) akiwa na kete 51 zinazosadikiwa kuwa ni madawa ya kulevya , kete hizo zilikua katika mfuko wa plastiki aliyokua ameubeba, jeshi la polisi limemkamata na hatua za kisheria zinaendelea juu yake.

16/06/2018, 6:20  mchana  hukohuko pujini dodo,jeshi la polisi limemkamata Yahya Abdalla Omar (20) akiwa na nyongo 11 zinazosadikiwa kuwa ni bangi .

17/06/2018, saa 3 asubuhi huko Mtambile jeshi la polisi lilimkamata Salah Mbarouk Salah ( 43  ) mkaazi wa kichungwani chakechake akiwa na kete 40 zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya.
Wito

Jeshi la polisi mkoa wa kusini Pemba linawataka wananchi hususan vijana , kuacha kabisa kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya kwani sheria zipo macho na zinamgusa kila atakaehusika.

Aidha Jeshi la polisi linawataka wananchi kuishi kwa kufuata misingi mema ya kimaisha yenye kuendana na sheria ili amani azidi kutawala kwa wote .


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.