Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Awata Mashehe Kuzuiya Upigaji wa Ngoma Katika Viwanja Vya Sikukuu.

Na Takdir Ali. Maelezo Zanzibar.                                   
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Muhammed Mahmoud amewaagiza Masheha kusimamia agizo la kuzuia upigwaji wa Ngoma katika viwanja vya sikuu ili kunusuru matatizo yanayoweza kujitokeza.
Amesema kuna baadhi ya Wananchi wamekuwa wagumu kutekeleza maagizo ya Serikali jambo ambalo haliteti ufanisi nzuri wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali iliojipangaia hivyo iwapo watakuwa mstari wa mbele kulisimamia suala la upigwaji wa Ngoma litaondoka kabisa.
Akizungumza na Waandishi wa Habari huko Afisini kwake Vuga Wilaya ya Mjini amesema uzoefu unaonyesha kuwa mikusanyiko ya Watu na kupiga Ngoma mara nyingi imekuwa ikileta viashiria vya uvunjifu wa Amani na utulivu ndani ya Mkoa huo.
Ameeleza upigwaji wa ngoma kwenye viwanja vya wazi vya sikukuu hikubaliki isipokuwa katika kumbi maalum za starehe na pia wafuate taratibu na sheria zilizowekwa ikiwa ni pamoja na kuanza saa nne za usiku hadi saa sita za usiku.
Akiitaja sabau ya kupiga marufuku kuwa ni pamoja na kutokana na uhalisia wa sikuu wenyewe kuwa ni ya Kidini, Kupunguza vitendo vya udhalilishaji kwa Wanawake na Watoto unaotokea katika viwanja vya kufurahishia watoto na kujikinga na uvunjifu wa Amani na utulivu.
Amefafanuwa ya kuwa katika Viwanja vyote vya Mkoa wa Mjini Magharibi vilivyoruhusiwa kufanya Sikuu wameweka Walinzi wa kutosha ili kuangalia utekelezaji wa maagizo yaliotolewa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na atakae kwenda kinyume atachukuliwa hatua za kisheria.
Mbali na hayo  Ayoub amewaagiza Masheha wa Mkoa huo kusimamia agizo hilo na yoyote atakaeshindwa Serikali ya Mkoa haitoshindwa  kumchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kumuajibisha.
                Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.