Habari za Punde

Mradi wa Tasaf Nchini Umwsaidia Kujenga Umoja wa Wazanzibar Bila ya Kujali Itikadi na Imani za Kidini.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Nd. Abdallah Hassan Mitawi akitoa neon la shukrani kwa Ujumbe wa Wakurugenzi wa Benki ya Dunia baada ya kukamilika kwa Tafrija waliyoandaliwa hapo Sea Cliff  Kama.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia pamoja na wale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Serikali ya Muungano wakiwa katika Tafrija ya pamoja ya kupongezana baada ya kumalizika kwa ziara ya Ujumbe huo wa Benki ya Dunia.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mihayo Juma N’hunga akibadilishana mawazo na Mmoja wa Wakurugenzi wa Benki ya Dunia wakipata chakula baada yakumaliza ziara ya Siku Tatu kukagua Miradi ya Maendeleo Visiwani Zanzibar.( Picha na – OMPR – ZNZ.)

Na.Othman Khamis OMPR.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdallah Hassan Mitawi alisema kwamba uwepo wa Mradi wa Tasaf Nchini umesaidia kujenga Umoja wa Wazanzibari bila ya kujali itikadi na imani zao za Dini.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Abdallah Hassan Mitawi wakati akitoa shukrani kwa Ujumbe wa Wakurugenzi wa Benki ya Dunia katika hafla iliyohudhuriwa pia na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hapo Hoteli ya Sea Cliff Kama.
Alisema tokea kuanza kwa Miradi hiyo wa Kaya Maskini Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania Awamu ya Tatu umesaidia kujenga Umoja na kuleta mwamko mpya  wa maendeleo chini ya program ya uwezeshaji wa Kaya hizo.
Akizungumzia umuhimu wa Mradi huo Naibu Katibu Mkuu huyo Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Mfuko huo umesaidia kupunguza Umaskini na kutoa fursa pana kwa Jamii kujiajiri wenyewe.
Ujumbe wa Wakurugenzi 80 kutoka Benki ya Dunia ulikuwepo Nchini Tanzania kwa ziara ya siku Tatu kukagua Miradiinayotekelezwa Nchini ambapo wameeleza kuridhika kwao na jinsi miradi hiyo inavyosimamiwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.