Habari za Punde

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC yatimiza miaka 20

Miaka  20  iliyopita mataifa 120 duniani yalitia  saini makubaliano  ya kuundwa  kwa  mahakama  ya  kimataifa  ya  uhalifu ICC. Hii ni Mahakama ya kuwaadhibu wahalifu, bila  kujali  utaifa  wa mtu aliyetenda uhalifu huo.

Hii ni  mahakama  inayotekeleza  sheria za kimataifa  na kuwaadhibu wahalifu , bila  kujali  wanatokea  wapi. Hilo ndio lilikuwa  wazo  la  msingi  la  kuundwa  kwa  mahakama  hii  ya  kimataifa ya  ICC. 
Niederlande - Internationaler Strafgerichtshof (Imago/P. Seyfferth)
Makao makuu ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague
Kilikuwa  ni  kikao  kilichokuwa  na  mvutano , Julai  1998  mjini  Rome. Ilichukua  miaka  mitatu  ya  malumbano  makali  katika  Umoja  wa mataifa  kuweza  kuunda  mahakama  hii  ya  kimataifa  ya  uhalifu   ICC mjini  The  Hague. Kikao  cha  siku  tatu  cha  kamati  maalum  ya baraza  kuu  la  Umoja  wa  mataifa  kilichoketi  kwa  muda  wa  siku tatu kilifanikisha  kupitishwa  kwa  azimio  la  baraza  kuu , kuhusiana  na mkataba  wa  kuundwa  mahakama  hiyo  ya  kimataifa.
Zilikuwa  juhudu maalum  za  waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa Ujerumani  wa wakati  huo Klaus Kinkel zilizofanikisha  kuundwa  kwa mahakama  hiyo  huru ya  uhalifu. Ilikuwa kutoka  mahakama  ya  Umoja wa  mataifa  ya  uhalifu  wa  kivita kwa  ajili  ya  iliyokuwa  Yugoslavia ya  zamani  na mahakama  ya  Umoja  wa  mataifa  ya  mauaji  ya kimbari  nchini  Rwanda, ambapo  mahakama  hizo  mbili ziliwekwa pamoja  na  kuunda  mahakama  ya  ICC.
Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa mataifa Kofi Annan akimwangalia waziri wa mambo ya kigeni wa italia Lamberto Dini akitia saini waraka wa kuanzishwa mahakama ya ICC Julai 18.Baraza la Usalama
Baraza  la  Usalama  la Umoja  wa  Mataifa iliifanya  mahakama  hiyo  mwanzoni  mwa  miaka ya  90  kuwa  chini  yake.
Baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa  liliteua  majaji  na waendesha  mashitaka  na  kuwa  na ushawishi  hadi  wakati  huo wa uwezekano wa  kuifunga  mahakama  hii wakati  wowote.  Kwa  kuwa ilitaka aina  nyingine  ya  mahakama  kama  hiyo.

Baraza  la  Usalama  lilitaka kuweka  azimio  la  kuichunguza  mahakama hiyo  na kuidhibiti. Lakini kutokana  na kushindwa  kwa  mataifa  kutimiza masharti  ya  kuingia  katika  mahakama  hiyo, baadhi  ya  mataifa yalizuiwa  kuingia  katika  mahakama hiyo. Mfano  ni  Libya  na Sudan.
Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu mjini The Hague Fatou Bensouda (katikati)
Kutokana  na  utata wa kisheria , ambao ni sheria  ya kutowajibika kisheria, Marekani  ilikataa kujiunga  na  mahakama  hiyo. Na iwapo ingejiunga  basi  wanajeshi  wa  Marekani  kutokana  na  kuhusika duniani  kote  kijeshi wangefikishwa  katika  mahakama  hiyo. Pia Marekani  ilikataa  suala  la  uchokozi, ambalo lilikuwa  ni  kosa kuishambulia  nchi  nyingine.
Mwandishi: Sabine Kinkartz / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri:Josephat Charo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.