Habari za Punde

Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na Maazimio ya Mkutano Mkuu wa 71 wa Afya Duniani.


MWAKILISHI wa Shirika la Afya Ulimwenguni Tanzania (WHO) Dkt. Adiele Onyeze akizungumza katika Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na Maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar.
NAIBU Waziri wa Affya Zanzibar Harus Said Suleiman akifungua Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar. 
NAIBU Waziri wa Afya Tanzania faustine Ndugulile, akionesha kipeperushi cha  Mpango kazi kilichoandaliwa na Wizara ya Afya Tanzania katika Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na Maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar. 
BAADHI ya Washiriki wa Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na Maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar.
BAADHI ya Washiriki wa Mkutano wa Marejesho wa Maamuzi na Maazimio ya Mkutano Mkuu wa (71) wa Afya Ulimwenguni katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngalawa Mjini Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir.-Maelezo - Zanzibar.
NAIBU  Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman  alisema  matarajio ya kuwapatia  wananchi huduma zilizo bora za afya  popote walipo ndio dhamira kuu ya Wizara zote za afya za Tanzania Bara na Zanzibar.
Hayo aliyasema  leo huko katika  ukumbi wa  Ngalawa Beach Resort wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mrejesho wa maamuzi  na maazimio ya mkutano  mkuu wa 71 wa Afya Ulimwenguni  .
Alisema Huduma za afya zinahitajika  kuwafikia wananchi  hivyo ili kufikia jitihada hizi Serikali zetu mbili hizi zimepiga hatua kubwa kuhakikisha kila sehemu zinawafikia walengwa bila matatizo yeyote na kwa urahisi.
Aidha alisema baada ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 nchi yetu imekuwa ikichukuwa kila jitihada ili kufikia malengo yaliyotarajiwa , hivyo nchi yetu imekuwa ni moja kati ya nchi chache Barani Afrika , zenye mtandao mzuri wa miundo mbinu ya Afya.
Amewahakikishia wananchi kuwa sasa huduma za Afya   za msingi zinapatikana katika masafa  yasiozidi kilomita nne hadi tano  hili ni jambo jema na tunapaswa kujipongeza.
Pia alisema Wizara na Serikali  imeweka kipaumbele kwa ujumla kuziimarisha zaidi huduma hizi  hasa katika maeneo na makundi maalum yakiwemo ya akinamama , watoto , walemavu  na wengine wenye mahitaji maalum.
“Serikali imedhamiria  kuziimarisha huduma za Afya nchini  kwa watu wa aina zote ili waweze kufaidika na fursa hizo”. Alisema Naibu Waziri huyo.
Alisema mipango tuliyonayo  katika kuimarisha Afya za jamii ni lazima kuangalia zaidi namna ya kuimarisha kinga ya maradhi yanayotuathiri kila siku , yakiwemo ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza .
Alielezea kinga ni bora kuliko kutibu hivyo ni vyema kuwekeza nguvu zaidi kwenye kinga kuliko kusubiri gharama kwa matibabu hapo baadae.
Vile vile alisema maradhi kama polio , surua, kipindupindu, malaria na mengine yanahitaji na mipango sahihi ya kupambana na kuimarisha viwango vya mafanikio  na hatimae kuyaondosha kabisa katika jamii , hili linawezekana tujitahidi kutimiza wajibu wetu.
Aidha alisema shirika la Afya Duniani WHO linahakikisha watu zaidi ya billion moja wananufaika huduma za afya , billion moja wanalindwa na dharura za afya na billion moja wanafurahia afya bora na ustawi mzuri wa maisha yao.
Nae Naibu  Waziri wa Wizara ya Afya Tanzania  Bara Dkt Faustine Ndegulile alisema anaridhishwa na mashirikiano yaliyokuwepo kati ya wizara za Afya hizi mbili kwa kwenda sambamba kuwajali wananchi wake katika upatikanaji mzuri wa huduma za Afya.
Alisema katika masuala ya Afya tunasaidiana , tunafundishana  kwa lengo la kukuza sekta hii ya Afya  kwa madaktari wa Zanzibar na Tanzania Bara ili kuweka kufikia katika malengo na mkakati uliyokusudiwa .
Pia alipongeza Zanzibar jinsi ilivyopiga hatua nzuri katika kudhibiti malaria, na kusema mipango zaidi  ya msingi yanaanza kufanyika ili kufikia kiwango kilokusudiwa, pia kuhakikisha dawa zinapatikana zinapatikana katika sekata zote mbili.
Sambamba  na hayo Afisa anayesimamia Malaria , Ukimwi , na Kifua Kikuu katika Shirika la Afya Duniani WHO Dr Ritha Njau alisema analipongeza shirika hilo kwa kuweza kudhibiti malaria kwa kutoa elimu ya wananchi kulalia vyandarua tayari vimetiwa dawa.
Vile vile aliwataka wananchi wakipata homa waende kupima kwa vile homa zote sio malaria  na hasa hivi sasa kasi za homa za malaria zimepungua .
Alielezea lengo la mkutano huu ni kuwapa  marejesho  wananchi  ambapo mara moja kwa mwaka hukutana  na kupanga mikakati kwa Bara na Visiwani.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.