Habari za Punde

Rais Dk Shein alipokutana na uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kikao cha siku moja cha Utekelezaji wa Mpango kazi wa Mwaka 2017/2018  na Mpango kazi wa Mwaka 2018-2019, kikao hicho kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]02/07/2018. 
Waziri wa   Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman alipokuwa akiwasilisha muhtasari wa Utekelezaji wa Mpango kazi wa Mwaka 2017/2018 katika kikao cha siku moja cha Uongozi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar  chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), akiwepo na Naibu Waziri Mhe.Khamis Juma Mwalim,[Picha na Ikulu.]02/07/2018. 

  Baadhi ya Maafisa katika Idara mbali mbali za Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakiwa katika kikao cha  utekelezaji wa mpango kazi wa mwaka wa fedha Juali-Juni 2017/2018 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,chini ya Mwenytekiti wake  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), [Picha na Ikulu.] 02/07/2018
Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Fadhil Suleiman Soraga (kulia) alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu suala la kuandama kwa Mwezi katika  Kikao cha Uongozi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais,Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora cha utekelezaji wa mpango kazi wa mwaka wa fedha Juali-Juni 2017/2018 kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,chini ya Mwenytekiti wake  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwepo na  Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana ZanzibarSheikh Abdalla Talib,[Picha na Ikulu.] 02/07/2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.