Habari za Punde

Wenye maradhi ya uti wa mgongo na vichwa vikubwa kupatiwa matibabu na madaktari bingwa kutoka Marekani


Na Mwashungi Tahir,   Habari Maelezo  Zanzibar  
     
WAZIRI wa Afya Hamad  Rashid Mohammed  amewataka wenye maradhi  ya uti wa mgongo na vichwa vikubwa wajitokeze  katika Hospital ya Mnazi Mmoja kwa wingi ili waweze kupatiwa matibabu  .
Akizungumza na madaktari bingwa wa maradhi hayo huko katika kitengo cha huduma hiyo alisema timu ya madaktari bingwa wa maradhi hayo wapo na watatoa huduma hiyo.
Alisema madaktari hao kutoka Marekani watafanya upasuaji kwa muda wa wiki moja kwa lengo la kuendeleza matibabu  na kuwaondoshea usumbufu wananchi kwa kufuatia huduma hiyo mbali.
“Tuhahihishe wenye maradhi makubwa kama hayo wajitokeze kwa wingi kuja kupatiwa matibabu “. Alisema Waziri huyo.
Pia alisema uko utaratibu maalum wa kila mwezi kuleta madaktari bingwa wa maradhi mbali mbali kuja Zanzibar kutoa huduma za matibabu kwa wananchi na kuwaomba waitumie fursa hiyo kila inapotokea.
Hamad alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais Dkt Ali Mohammed Shein inajitahidi kuimarisha sekta ya Afya ili wananchi wake wapate huduma kwa urahisi bila ya gharama kwa lengo la kuwa na afya bora.
Alisema kuwa sehemu za huduma ziko na zinatolewa kwa wananchi bila ya matatizo yeyote na aliwahakikishia wananchi kuimarishwa sehemu ya viungo ili nayo itoe huduma.
Aidha alisema madaktari wengine wako Pemba kwa kutoa huduma za upasuaji na kuimarisha huduma za mama na mtoto ili kupata makuzi bora mtoto  na afya bora kwa mama .
Vile vile aliwaomba vijana wajifunze taaluma hizi ili wakiondoka madaktari hao bingwa wao waweze kuendeleza hasa manesi baada ya daktari kufanya upasuaji mgonwa ni vizuri awepo nesi karibu kwa ajili ya kumpa huduma mgonjwa.
Nae mratibu wa kitengo hicho cha upasuaji wa vichwa vikubwa uti wa mgongo Dr  Mohammed Ali Haji alisema timu ya madaktari kutoka Marekani, Spain na Abudhabi wapo kwa ajili ya kutoa matibabu kwa wananchi wenye maradhi hayo.

Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.