Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt Ramadhani Kitwana Dau (kulia) mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta Indonesia leo, akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Viongozi mbali mbali,katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla,[Picha na Ikulu.]31/07/2018.
Katika uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Indonesia, Soekarno- Hatta, uliopo mjini Jakarta Dk. Shein
alipokelewa na miongoni mwa viongozi wakuu wa Serikali wa Nchi pamoja na Balozi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia ambaye pia anaiwakilisha
nchi hiyo Ramadhan Dau.
Ziara hiyo ya Dk. Shein
ambayo inatarajiwa kuanza rasmi hapo
kesho itaanza kwa mazungumzo na mwenyeji
wake Makamo wa Rais wa nchi hiyo Muhammad Jusuf Kalla na baadae kufanya
mazungumzo na viongozi wengine mbali mbali wa ngazi za juu wa Serikali pamoja na
viongozi wa sekta binafsi wa nchi hiyo.
Katika
ziara hiyo, Rais Dk. Shein amefuatana na viongozi mbali mbali akiwemo Mke wa
Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko,
Balozi Amina Salum Ali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Issa, Haji Ussi Gavu, na viongozi wengine wa Serikali.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein anatarajiwa
kufanya ziara nchini humo ambayo atakutana na viongozi wakuu, kutembelea miradi
mbalimbali ya maendeleo, kukutana na wafanyabiashara, kutembelea sehemu za
utamaduni na zile za kitalii.
Dk.
Shein anatarajiwa kurejea nchi Agosti 6, mwaka huu.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar.
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment