Habari za Punde

Wanaopasi vizuri waandaliwe mazingira mazuri ya masomo ya juu

Na, Khaleed GWIJI.

Kwanini kusianzishwe mpango kabambe, makhsus na wenye dira ya muda mrefu kwa wanafunzi wa Zanzibar wanaopasi vizuri sana kuwataftia udhamini wakusoma vyuo vikuu vya nje vilivyo na ubora (highly respected institutions) ambavyo vimekuwa grouped under the label ya ‘Ivy League’ — vyuo ambavyo strongly serves students for professional careers ambapo kwa muktadha na mahitaji ya kwetu basi ni vyema zaidi tukaekeza kwenye fani za degree in fisheries and aquaculture, medicines, petroleum engineering, paediatric nursing, bachelor of science in agriculture, food business management degree program, math and statistics, computer and information sciences, communication technologies, law, etc.

Kufanikisha hilo ni pamoja na kuwaandaa wanafunzi wa Kizanzibari kuweza kufaulu katika standardized tests kama TOEFL, IILSES, test scores (SAT, GRE, LSAT), GPA, pia kuweza kupasi katika interviews, kuandika essays na kujaza application forms ipasavyo, na kupata watu Zanzibar au nje ya Zanzibar wenye ujuzi wa kuandika recommendation letters kwa mujibu wa viwango vinavyotakiwa na vyuo vikuu hivyo vyenye ubora pamoja na kupata vibali vya utambulisho kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) na other academic achievements.

Ni muhimu kupatikane taasisi ndani ya Zanzibar ambayo itakuwa na highly and reliable professionals ambao wataweza kuyafanikisha hayo kwa vijana wa Kizanzibari walio weledi na wenye vipaji au hata kuingia ubia na chuo kikuu bora kilichopo nje ya Zanzibar kuweza kulifanikisha hilo. Hapo panahitajika uongozi thabit, sera makini na fedha za kutosha na kwa wakati ili kuifanikisha ndoto nzuri kama hiyo. 

Hayo yanahitajika kwa sababu admission katika vyuo hivyo ni highly competitive, na ili wanafunzi wakubaliwe ni lazima wawe wamefikia viwango vya juu ukilinganisha na any average public university. Tukiyaweza hayo, maana yake baada ya miaka 10 usoni insha’Allah Zanzibar itakuwa na kundi kubwa na teule lenye elimu nzuri sana litakalofanya maajabu katika harakati za maendeleo ya kuijenga Zanzibar kwa faida yetu sote.

Njia moja wapo ya kuhakikisha vijana hao wanarudi kuja kuitumikia Nchi yao ya Zanzibar baada ya kuhitimu, ni kuwepo kwa utaratibu maalum wa mikataba (binding contracts) itakayowataka wanafunzi hao baada ya kumaliza masomo yao nje kurudi nyumbani na kuja kutumia elimu zao kwa maslaha mapana ya Zanzibar na watu wake kwa muda utakaokubaliwa na kuainishwa ndani ya mikataba hio na baada ya kumaliza muda huo wawe na fursa ya kuchagua kuendelea kuitumikia Zanzibar au kwenda nje au kufanya yote mawili.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.