Habari za Punde

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Afungua Mafunzo ya Madaktari Kisiwani Pemba.


Na.Shaib Kifaya - Pemba..
Waziri w Afya zanzibar ,Hamad Rashid Muhammed ,amesema suala laa kuwajengea uwezo kwa madaktari wa Hospital mbali mbali ni jambo la msingi kwani kutawaongezea uwelewa na kumudu kazi zao na kuwahudumia wagonjwa wanaofika hospitalini kwa kupatiwa matibabu.

Kauli hiyo, aliitoa huko Hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani, wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya ya wiki moja kwa Madaktari wa Hospital tano Kisiwani Pemba.

Alisema lengo la mafunzo hayo ni kupunguza vifo kwa watoto chini ya umri miaka mitano pamoja na kupatiwa matibabu sahihi kwa watoto .

“ Mafunzo hayo yanayotolewa na madaktari  wetu   wa Kichina yatawajenga uwezo licha ya kwamba Chuoni wamesha soma “alisema Waziri.

Aliwataka madaktari hao kuyapokea kwa usahihi mafunzo kwani ni muhimu sana kutokana na utoaji wa huduma kwa wagonjwa kutoka kila kada wanazozitumia kutoa huduma .

Nae Ofisa mdhamini Wizara ya Afya Pemba, Shadya Shaabani Seif,alisema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwa madaktari  hao ili kuona wanatoa huduma zilizo  bora na za usahihi.

Mdhamini huyo ,aliipongeza timu ya mkupuo wa 28 ya madakatri wa Kichina , ambao walipokelewa rasmi hivi karibuni hapo Abdalla Mzee Hospitali, kwa kuwa na moyo wa uzalendo wa kuwandaa mafunzo hayo ya kuwahenga uwezo madaktari  kwa kuboresha utendaji wa majukumu yao .

Hata hivyo alisema atashirikiana na timu  ya madaktari  hao pamoja na uongozi wake wa Wizara ili kuona wanaushirikiano  mzuri na kuzitatua changamoto ambazo zitawakabili.

Nae Kiongozi wa timu  ya Madaktari  wapya wa Kichina Dk, Cao Wei ,alimpongeza waziri wa Afya Zanzibar kwa mapokezi mazuri aliwapokea tangu kingia Kisiwani Zanzibar na hadi sasa na alimuahidi kufanya kazi vizuri kwa kipindi chote cha kazi watakapo kuwepo .

‘’tunamshukuru Waziri kwa mapokezi mazuri mliotuonyesha basi na  sisi tunakuwahidi kufanya kazi kwa mashirikiano “ alisema.

Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo, alisema ni utaratibu wao ambao hufanya kila wanapofika kuwapatia madaktari ili kuongeza uwelewa na kuboresha huduma kwa wanajamii wanaofika Hospitali kupatiwa natibabu.

“ Mafunzo haya yamelenga kwa Madaktari  wanaotoa huduma wodi ya watoto na wakunga  kwa lengo la kupunguza vifo kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano”, alisema

Mafunzo hayo ya wiki moja yamedhaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China na yamewashirikisha madaktar 28 kutoka Hospital ya Abdalla Mzee Mkoani ,Chake Chake,Vitongoji,  Wete na Micheweni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.