Habari za Punde

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Kangi Lugola Ziarani Jijini Arusha leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto), akiongozana na Naibu Waziri  Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (kulia) na  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wapili kulia), kutembelea eneo la Kaloleni zilipo nyumba za polisi, jijini Arusha.
Waziri  wa Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi,  Kangi Lugola (wapili kushoto),  akimsikiliza Kamanda wa  Polisi  Mkoa  wa  Arusha, Ramadhani  Ng’anzi (kulia) baada ya kutoka kutembelea Kituo cha Polisi Utalii.Wapili  kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimsikiliza mmoja wa wananchi waliofika Kituo cha Polisi kupata huduma,Waziri Lugola yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi
 Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na mdau wa maendeleo mjini Arusha,Hans Pol.Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo.Waziri Lugola yupo mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, Naibu Waziri  Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (kushoto)  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia),wakisikiliza taarifa ya Kituo cha Polisi Utalii baada ya viongozi hao kutembelea kituo hicho.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.