Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar Yawazawadia Wanafunzi Waliofanya Vizuri Mitihani Yao ya Kidatu Cha Sita Unguja na Pembe.

Naibu Mkurugenzi Ntendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd PBZ B. Khadija Shamte Mzee akizungumza na kuwapongeza Wahitimu wa Wanafunzi wa Skuli za Unguja na Pemba waliofanyika vizuri na kupata ufaulu mzuri wa daraja la kwanza katika mitihani yao kwa mwaka wa masomo 2017/2018. wakati wa hafla iliofanyika katika viwanja vya kariakoo Zanzibar kukabidhiwa fedha zao zilizotolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Green Light Foundation Ndg.Salim Mussa Omar akizungumza na kutowa historia ya Taasisi yao iliojitolea kuinua Elimu katika Visiwa vya Unguja na Pemba, akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi Wanafunzi waliopata Daraja la Kwanza Mitihani yao Kidatu cha Sita 2017/2018. 
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Idrissa Muslim Hija akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wahitimu wa Mitihani ya Kidatu cha Sita 2017/2018 wakati wa hafla ya kukabidhizwa zawadi zao za fedha zilizotolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ katika viwanja vya Watoto Kariakoo Zanzibar.kushoto Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Bi. Khadija Shamte Mzee na kushoto Mkurugenzi wa Green Light Foundation Salim Mussa Omar .Akitowa neno la shukurani mwanafunzi Mmoja wa Mwanafunzi wa Kidatu cha Sita Biubwa Khamis aliahidi kwamba fedha walizokabidhiwa zitatumika zilivyokusudiwa sambamba na kuja kulitumikia taifa mara baada ya kumaliza masomo yao 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.