Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar Bi. Khadija Shamte Mzee alizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wanafunzi Wahitimu wa Kidatu cha Sita Zanzibar wakati wa kukabidhiwa zawadi zilizotolewa na Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ katika viwanja vya Watoto Kariakoo Zanzibar. ,
Naibu Mkurugenzi wa PBZ,Bi.Khadija Shamte Mzee aliahidi kwamba
utoaji wa zawadi kwa wanafunzi wanaofaulu vyema itakuwa endelevu kwani
imedhamiria kujenga taifa lenye rasilimali watu wenye ujuzi na utaalamu utakao saidia kuleta mabadiliko
ya haraka kiuchumi.
Alisema ulimwengu wa sasa unahitaji wasomi na wataalamu wengi hivyo
aliwashauri kujifunza elimu ya matumizi ya fedha na kujiandaa na bajeti hasa
ikizingatiwa ndio msingi wa maisha ya mwanadamu katika kujipangia hatua za
kimaisha.
Aliwahimiza kufuata maadili na kujiheshimu wakati wote wanapokuwa
katika masomo kwani ni miongoni mwa mambo yatakayowasaidia kutimiza ndoto zao.
Katika sherehe hiyo wanafunzi waliopata daraja la 1.3 walikabidhiwa
shilingi milioni 3,000.000 kila mmoja ambapo wanafunzi waliopata daraja la 1.5
walipatiwa shilingi milioni 1.5 na wengine wa daraja la 1.6 hadi 9 walipatiwa
shilingi milioni 1,000,000.
No comments:
Post a Comment