Habari za Punde

IGP Simon Sirro Akiendelea na Ziara Yake Mkoani Arusha

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Maofisa waliopo Shule ya Polisi Moshi zamani CCP wakati wa ziara ya kikazi kuangalia mwenendo wa mafunzo chuoni hapo na kuzungumza na Wakufunzi wa chuo hicho
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua gwaride baada ya kuwasili Shule ya Polisi Moshi zamani CCP kwa ziara ya kikazi kuangalia mwenendo wa mafunzo chuoni hapo na kuzungumza na Wakufunzi wa chuo hicho.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi Hamis Issah na RPC Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ramadhan Nganzi wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Wakazi wa Kata ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli wakati alipokwenda kuzungumza nao wakati wa Ziara yakeya kikazi Mkoa wa Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro pamoja na Afisa Mtendaji wa Kata ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli Bi Kuluthum Hassan wakikagua eneo la Polisi linalotarajiwa kujengwa kituo cha Polisi wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoani Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Ramadhan Nga’nzi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi. Theresia Mhongo wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoani Arusha yenye lengo la kutatua changamoto za uhalifu (Picha na Jeshi la Polisi).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.