Habari za Punde

Kikwete amjulia hali Dkt. Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI

Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla kitengo cha mifupa MOI anapopatiwa matibabu. Kulia ni Mke wa Waziri Dk Kigwangalla, Dkt. Bayoum Awadhi Kigwangalla.
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Andrew Chale ambaye ni Mwandishi wa Habari Maalum wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla. Kulia ni Dkt. Bayoum Awadhi Kigwangalla mke wa Waziri  Dkt.Kigwangalla.

Na Andrew Chale, Dar
Rais Mstaafu wa awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano 
wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya tarehe 14, 
Agosti 2018 amemtembelea na kumjulia hali Waziri wa 
Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla aliyelazwa 
katika wodi maalum kitengo cha Taasisi ya mifupa 
MOI,  hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Kikwete kumtembelea Dk 
Kigwangalla ambapo awali alimtembelea Agosti 
8,  alipokuwa amelazwa Wodi ya Mwaisela akipatiwa 
Matibabu ya awali.

Kikwete amemtakia kila lakheri katika kipindi hiki kwa 
kuuguza majeraha ya mkono na sehemu za mwili ikiwemo 
mbavu ambazo kwa sasa hali yake inaendelea kuimarika kwa 
majibu wa Madaktari wa kitengo hicho cha mifupa MOI.

Awali tokea kufanyiwa operesheni ya mkono ameweza 
kufanya mazoezi taratibu ikiwemo kutembea mwenyewe 
katika viunga hivyo vya Muhimbili.

Dkt. Kigwangalla alipata ajali ya gari mnamo Agosti 4, 2018 
huko Manyara akiwa katika ziara ya kikazi ambapo katika 
ajali hiyo iliyokuwa na watu 6, watano walijeruhiwa na 
mmoja alifariki dunia ambaye alikuwa afisa habari 
mwandamizi wa Wizara hiyo, Hamza Temba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.