Habari za Punde

Klabu ya Man United Iko Mbioni Kumtangaza Mkurugenzi Wake wa Michezo

Golikipa wa zamanI wa Man United Edwin Van De Sar anatajwa kuwa na nafasi kubwa kuwa mkurugenzi wa michezo.

Klabu ya Man United iko katika mpango wa kumtangaza Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo baada ya klabu hiyo kushindwa kufanya vyema katika dirisha kubwa la usajili
Katika mchakato huyo naibu mwenyekiti mtendaji wa United Ed Woodward atashirikiana kocha Jose Mourinho kumpata Mkurugenzi huyo wa michezo
Tayari majina matatu yanatajwa kuweza kupewa nafasi hiyo ambao ni Golikipa wa zamani wa timu hiyo muholanzi Edwin Van Der Sar
Pia yupo mkurugenzi wa michezo wa As Roma Muhispania Ramón Rodríguez Verdejo maarufu kama Monchi pamoja na Fabio Paratici
Mkurugenzi wa michezo wa As Roma Ramón Rodríguez Verdejo maarufu kama Monchi pia anapigiwa upatu wa kupewa kazi na Man United.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.