Habari za Punde

Mkutano Mkuu wa Nne wa Wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, na Kuadhimisha Miaka 20 ya Mfuko Huo Tangu Kuazishwa Kwake Zanzibar.

Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico akizungua Mtandao wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Mobile App kuwarahisishia Wanachama wa Mfuko huo kupata taarifa za Mafao yao kupitia simu zao za kiganjani kushoto Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSSF Bi. Sabra Issa Machano na kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZSSF Dkt. Suleiman Rashid wakishududia uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbe wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Bi. Sabra Issa Machano akitowa maelezo ya maendeleo ya Mfuko wa ZSSF kwa Wadau wakati wa hafla ya Mkutano Mkuu wa Nne wa ZSSF, uliokwenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 20 ya Mfuko huo tangu kuazishwa kwake na changamoto uliokutana nazo na mafanikio ya mfuko huo katika kuazisha kwa Mirandi mbalimbali ya maendeleo kwa Wananchi wa Zanzibar.
Waziri wa Kazi Uwezeshaji wa Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Castico akifungua Mkutano Mkuu wa Nne wa Wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, ikiwa sambamba na kuadhimisha miaka 20 ya Mfuko huo tangu kuazishwa kwake, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. 
Maofisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nne wa Wadau na Uzinduzi wa Mtandao wa ZSSF Mobile App, uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Nne wa Wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Mameneja wa Mabenki Tanzania Wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa ZSSF na Uzinduzi wa Mtandao wa ZSSF Mobile App kwa Wanachama wao kupata habari na taarifa za michango yao kupitia katika App hiyo.
Katibu Mkuu wa ZATAC Ndg. Khamis Mwinyi akitowa salamu za Chama cha Wafanyakazi Zanzibar ZATUC wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nne wa Wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Mwakilishi wa ZANEMA Ndg. Ali Aboud akitowa salamu za Chama cha Waajiri Zanzibar (ZANEMA)wakati wa hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nne wa Wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Viongozi wa meza kuu wakifuatilia maelezo ya Wadau wa ZSSF Wawakilishi wa Mabenki yanayoshirikiana na Mfuko huo kulipa mafao ya Wanachama wao. 
Senior Manager Retail & Banking Azania Bank Ndg. Jackson Lohay akizungumza na kutowa maelezo ya huduma ya Benki yao inayotowa fursa kwa Wateja wao na Wastaaf kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF na wateja wengine wanaotumia benki yao. akizungumza wakati wa hafla ya Mkutano Mkuu wa Nne wa ZSSF uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Mkurugenzi wa Masoko wa Benki ya Posta Tanzania Tpb Ndg. Henry Bwogi akizungumza na kutowa maelezo ya huduma ya Benki yao inayotowa fursa kwa Wateja wao na Wastaaf kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF na wateja wengine wanaotumia benki yao. akizungumza wakati wa hafla ya Mkutano Mkuu wa Nne wa ZSSF uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Meneja Muandamizi wa Taasisi za Kiserikali Makao Makuu Benki ya NMB Ndg. Stephen Chavallah, akizungumza na kutowa maelezo ya huduma ya Benki yao inayotowa fursa kwa Wateja wao na Wastaaf kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF na wateja wengine wanaotumia benki yao. akizungumza wakati wa hafla ya Mkutano Mkuu wa Nne wa ZSSF uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.

Afisa Muandamizi Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd 9PBZ) Ndg. Anasi Ramadhan Rashid,azungumza na kutowa maelezo ya huduma ya Benki yao inayotowa fursa kwa Wateja wao na Wastaaf kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF na wateja wengine wanaotumia benki yao. akizungumza wakati wa hafla ya Mkutano Mkuu wa Nne wa ZSSF uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
Mwanasheria wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Ndg. Ramadhani Juma Suleiman akiwasilisha Mada ya Mfuko wa ZSSF kwa Wadau wakati wa Mkutano Mkuu wa Nne wa ZSSF uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.