Habari za Punde

Mwandishi wa Habari za Michezo Visiwani Zanzibar Ateuliwa Kuwa Msemaji wa Kamati ya ZFA Zanzibar.

Kamati teule inayosimamia shughuli zote za Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) imepata msemaji wao mpya ambae ni Abubakar Khatib Kisandu muandishi na mtangazaji wa michezo wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).
Akithibitisha kuteuliwa kwake Kisandu amesema kweli amepokea barua kutoka kwa Katibu msaidizi wa kamati hiyo Muhamed Hilali Tedy ya tarehe 7 mwezi Agost yenye namba ZFA/KM/141/VOL/4 kutoka ofisi ya ZFA Taifa.
Aidha Kisandu amekubali uteuzi huo na kuwaomba wadau wa michezo kumuunga mkono kwenye kipindi chote cha miezi sita ya utumishi wake ndani ya kamati teule hiyo kwa kuwa wapo kwenye kipindi cha kusimamia mpira wa Zanzibar.
Kwa Upande mwengine kisandu amewataka wandishi wenziwe wa michezo kuumpa ushirikiano kwa kuwa yupo katika majukumu mazito ya kitaifa ya kuusemea mpira wa Zanzibar ambao kimsingi umekuwa na Changamoto nyingi sana.
“Nafurahi uteuzi huu kwa kuwa ni mwanamichezo na muomba mungu anisaidie kwenye jukumu hili na nawaomba sana wandishi wa michezo na wandishi wote waniunge mkono sisi ndio wenye dhamana ya kufikisha mbali mpira wetu” Alisema Kisandu.
Abubakar Kisandu amengia kwenye orodha hii ya wateule wajumbe na kubeba nafasi ya msemaji wa kamati hiyo teule, kabla ya hapo ZFA ilikuwa na msemaji Ali Bakari Cheupe ambae alikuwa anafanya kazi zote za Afisa Habari wa Chama hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.