Habari za Punde

Naibu Waziri Mhe Japhet Hasunga Awataka Wawekezaji Kwenye Hifadhi Tano Zilizorudishwa Hadhi.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( katikati) akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wakati alipowasili katika ofisi za wilaya ya Karagwe kabla ya kutembelea jana pori la akiba Kimisi  katika ziara yake ya siku tatu  mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika  pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa,  Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Karagwe, Godfrey Luheluka
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga  akisaini kitabu cha wageni mara  alipowasili katika ofisi za wilaya ya Karagwe kabla ya kutembelea jana pori la akiba Kimisi  katika ziara yake ya siku tatu  mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA  katika  pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ngala pamoja na baadhji ya watumishi wa TAWA na TANAPA wakati Naibu Waziri huyo  alipotembelea jana pori hilo katika ziara yake ya siku tatu  mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika  hilo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto)  akioneshwa ramani inayoonesha Ziwa Ngozi ambalo ni miongoni mwa vivutio vya utalii katika Pori la Akiba la Kimisi na aliyekuwa Meneja wa Pori hilo Bigilamungu Kagoma   wakati Naibu Waziri huyo  alipotembelea jana  pori hilo katika ziara yake ya siku tatu  mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA  katika  pori hilo lililopandishwa hadhi kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa
 (Picha na Lusungu Helela -WMU)

Na. Lusungu Helela - Kagera.
Baada ya kuyapandisha hadhi mapori matano ya akiba, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amewataka  wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kuwekeza katika Mapori hayo.

Aidha, Amesema  Serikali imefuta kodi ya kuingiza magari ya watalii nchini  ili kuwawezesha wananchi walio wengi kuingia katika biashara hiyo ikiwa lengo ni kuongeza mapato ya Serikali kupitia sekta ya Utalii.

Ametaja aina ya uwekezaji unaohitajika kuwa ni ujenzi wa hoteli zenye hadhi ya nyota moja hadi zenye nyota tano, nyumba za kulala wageni, uanzishwaji wa makampuni ya utalii pamoja na kutoa huduma za vyakula kwa ajili ya  watalii.

Ametoa rai hiyo leo wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani Karagwe mkoani Kagera kabla ya  kutembelea ziwa Ngoma ambalo ni miongoni mwa vivutio vya utalii vilivyopo katika Pori la Akiba la Kimisi ambalo ni miongoni mwa mapori yaliyo katika mchakato wa kuwa hifadhi za taifa.

Naibu waziri huyo anatembelea mapori ya mkoa wa Kagera kufuatilia hatua iliyofikiwa na Hifadhi za Taifa Tanzania ( TANAPA)katika kuyaendeleza.

Amesema Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika ni hazina na fursa kwa mikoa ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania kufunguka kiutalii kwa wananchi wa maeneo hayo na taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.