Habari za Punde

Polisi Kilimanjaro Yanasa Kilogramu 520 za Mirungi.

Mtuhumiwa wa usafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi akiwa kwenye gari la Polisi ba Viroba vilivyojaa Dawa hizo zilizokamatwa katika moja Bonde mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Asakari Polisi wakishusha viroba vyenye Dawa za Kulevya aina ya Mirungi.
Mtuhumiwa wa usafirishaji wa Dawa za kulevya aina ya Mirungi,Samwel Muro mkazi wa Kitobo nchini Kenya akiwa chini yaulinzi na pemebeni ake ni Vifurushi vya Mirungu alivyokutwa navyo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akitoa maelekezo kwa askari wake mara baada ya kukamatwa kwa Dawa za kulevya aina ya Mirungi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akiumuuliza jambo raia wa Kenya ,Samwel Muro aliyekutwa akiwa amebeba moja ya vifurushi kwa ajili ya kusafirihwa kutoka mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah akionesha moja ya kifurushi cha Dawa za kulevya aina ya Mirungi kilichopewa jina la mji wa Kibaha.

Na Dixon Busagaga  wa Globu ya Jamii kanda ya Kaskazini.

JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limefanikiwa kukamata viroba saba vya Dawa za kulevya aina ya Mirungi sawa na kilogramu 520 zikiwa zimebebwa na watembea kwa miguu ambao walikuwa wakivusa kutoka nchi jirani ya Kenya kuingia Tanzania.

Mbali na viroba hivyo ,Polisi pia inamshikilia mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la ,Samwel Muro(21) raia wa Kenya mkazi wa Kitobo baada ya kukutwa akiwa amebeba kichwani moja ya Viroba hivyo huku wakifanikiwa kuwakimbia askari baada ya kutupa mizigo ya dawa hizo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna  Msaidizi wa Polisi,Hamis Issah alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo  jana majira ya 8:30 mchana pamoja na pikipiki moja iana ya Haojue yenye namaba za usajili MC 909 BUZ  ambayo inatajwa kuhusika katika usafirishaji wa mizigo hiyo.

“Hii mirungi ilikamatwa kijiji kinaitwa Mnoa ,kiko kata ya Kileo wilayani Mwanga ,askari Polisi wakiwa Doria walikamata viroba saba vya mirungi ,asakri walienda kwenye bonde moja na kukuta watu wametoka Kenya ,wamejiza hii mirungi kwenye magunia wanaficha kwenye hilo bonde ,kumbe wana utaratibu wao bonde likijaa wanachukua pikipiki zaidi ya 30 kwa ajili ya kusafirisha na wanasafiri kwa makundi makubwa ya pikipiki”alisema Issah.

Kamanda Issah alisema baadhi ya Vifurushi hivyo vya Mirungi vimekutwa vikiwa vimeandikwa majina ya vijiji kuanzia njia Panda ya Himo kuelekea Dar es Salama yakiwemo maeneo ya Segera ,Chalinze hadi Kibaha.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.