Habari za Punde

Rais Dk Shein afanya ziara katika taasisi za kitafiti

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohammed Shein katikati akipatiwa maelezo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Zanzibar(ZALIRI)Dk,Kassim Gharib Juma kuhusiana na ramani ya majengo ya utafiti katika ziara alioifanya kuangalia Maendeleo ya Taasisi hio Dole Langoni Magharibi A Unguja.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohammed Shein wapili kushoto  akipatiwa maelezo na Mtafiti wa Magonjwa na Uzalishaji wa Mifugo Dk,Waridi Abdalla Mussa kuhusu uzalishaji wa Kuku wa Kienyeji katika ziara alioifanya kuangalia Maendeleo ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Zanzibar(ZALIRI) Dole Langoni Magharibi A Unguja.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohammed Shein katikati akitembelea eneo linalotarajiwa kujengwa Hospitali ya Rufaa  alipofanya ziara ya kuangalia mipaka ya eneo hilo Binguni Wilaya ya Kati Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk,Ali Mohammed Shein akizungumza na Wananchi waliohudhuria katika eneo linalotarajiwa kujengwa Hospitali ya Rufaa  alipofanya ziara ya kuangalia mipaka ya eneo hilo Binguni Wilaya ya Kati Unguja.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

A Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 29.08.2018
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amesema azma ya serikali anayoiongoza ni kuhakikisha kuwa tafiti za Mifugo na Afya zinafanyika Zanzibar badala ya kufanyika nje ya Zanzibar.
Amesema kuundwa kwa Taasisi za kitafiti na kujengewa uwezo Taasisi hizo ni hatua muhimu itakayo chochea kasi ya maendeleo na kupunguza gharama.
Rais Shein ameyasema hayo alipofanya ziara katika eneo la Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Dole Wilaya ya Magharibi A na eneo la Binguni ambapo Hospital ya Rufaa itakayojumuisha Taasisi ya Utafiti ya Afya inajengwa.
Akiwa katika Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Dkt Shein ameridhishwa na maendeleo ya Taasisi hiyo ikiwemo ukarabati wa majengo mbalimbali na shughuli za kitafiti zinazoendelea katika Taasisi hiyo.
Dkt Shein alijionea Tafiti zinazoendelea katika Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na ufugaji wa kuku wa Kienyeji na chakula cha Samaki.
Aidha ameahidi kuendeleza mashirikiano yake kwa Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kusaidia kuiwezesha kifedha ili kukidhi bajeti ya Taasisi hiyo.
Akiwa Binguni Dkt. Shein aliweza kukagua mipaka ya eneo ambalo Hospital ya kisasa ya Rufaa inatarajiwa kujengwa.
Amezitaka Taasisi zinazohusika na eneo hilo kuhakikisha wanafanya marekebisho ya upimaji wa eneo hilo ili kurahisisha ujenzi wa Hosptiali hiyo.
Ujenzi huo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambapo Dkt Shein aliahidi kuijenga Hosptal hiyo katika mikutano ya kujinadi kuchaguliwa.
Akielezea kwa undani Dktk Shein amesema Tayari Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshaomba Fedha za Mkopo na kwamba kila kitu kimeenda sawa hivyo ujenzi unaweza kuanza mara tu fedha zitakapopatikana.
Dkt Shein amewataka Wananchi kujitolea kwa hali na mali ili kufanikisha ujenzi huo pale utakapo anza.
Katika Ujenzi huo kutakuwa na Hospital ya Rufaa na Taasisi ya Utafiti wa Afya na nyumba za Wafanyakazi.
Awali akitoa Salamu za Kichama Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Dkt Abdallah Sadala amempongeza Dkt Shein kwa kuendelea kuitekeleza vyema Ilani ya CCM kama alivyoahidi kwa wananchi na hivyo kuomba wananchi waendelee kumuunga Mkono.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.