RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za
pongezi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya India Narendra Damodardas Modi, kwa
kuadhimisha miaka 72 tokea Taifa hilo kupata huru wake.
Salamu hizo zilieleza kuwa wananchi wa Zanzibar
wanaungana na ndugu zao wa Jamhuri ya India katika kusherehekea sikukuu hiyo
adhimu ya uhuru wa Taifa hilo ambayo ambayo ni ya kihistoria.
Katika salamu hizo, Dk. Shein alimuhakikishia Waziri
Mkuu huyo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendeleza uhusiano na
ushirikiano wa kihistorin uliopo kati yake na India sambamba na kuvumbua maeneo
mapya ya mashirikiano kwa maslahi ya pande zote mbili.
Dk. Shein alimtakia kiongozi huyo na familia yake pamoja
na wananchi wote wa India afya njema na sherehe njema katika kuadhimisha siku
hiyo ya adhimu kwa Taifa hilo na kumtakia mafanikio zaidi ya kiuchumi kwa
madhumuni ya kulinufaisha Taifa hilo na wananchi wake kwa amani na utulivu
mkubwa.
Jamhuri
ya India inasherehekea siku ya uhuru wa Taifa hilo kila ifikapo Agosti 15 ya
kila mwaka ambapo nchi hiyo ilipata uhuru wake kutoka kwa Wakoloni wa Kiengereza
mnamo mwaka 1947 chini ya uongozi wa muasisi na Baba wa Taifa hilo Hayati Mahtma
Gandhi.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address:
2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment