Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Aweka Jiwe la Msingi na Kulizindua Jengo la Treni Darajani Baada ya Kumalizika Ujenzi Wake Mkubwa wa Maduka ya Kisasa na Nyumba za Makaazi

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsalimia na kuzungumza na Bi. Zuwena Salum Said aliyekuwa mkaazi wa jengo hilo la Treni, wakati hafla hiyo ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi na Kulifungua Rasmin kutowa huduma kwa Wananchi wa Zanzibar kwa kukodisha Fremu za Maduka na Nyumba za Makaazi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa  Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZSSF Bibi.Sabra Issa Machano (katikati) mara baada ya kulifungua  Jengo la "Chawi" maarufu Jumba la Treni liliopo Dajani Mjini Zanzibar lililofanyiwa matengenezo makubwa na Kampuni ya CRJE kutoka  China katika sherehe zilizofanyika leo,


Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSSF Sabra Issa Machano akitoa hotuba na kuelezea historia ya jengo la Treni  (CHAWL BULDING) lililofanyiwa matengenezo na ZSSF na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein darajani mjini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake kwa Viongozi na Wananchi waliohudhuria katika sherehe za ufunguzi wa  Jengo la "Chawi" maarufu Jumba la Treni liliopo Dajani Mjini Zanzibar baada ya kulifuingua leo,ililofanyiwa matengenezo makubwa na Kampuni ya CRJE kutoka  China


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.