Habari za Punde

TANAPA Yatenga Bilioni 3.9 Kuendeleza Hifadhi Tano Zilizopandishwa Hadhi na Kuwa Hifadhi za Taifa Tanzania.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto)  akioneshwa mpaka kati ya Pori la Akiba la Burigi na eneo la wananchi katika eneo la Nyungwe na Ofisa mwenye wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi  aliyeteuliwa na Hifadhi za Taifa Tanzania kusimamia Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa, Damian Saru ( wa kwanza kulia) wakati Naibu Waziri huyo  alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu  mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika  mapori hayo,  Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto)  akioneshwa mpaka kati ya Pori la Akiba la Burigi na eneo la wananchi katika eneo la Nyungwe na Meneja wa  Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa , Bigilamungu Kagoma  ( wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri huyo  alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu  mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika  mapori hayo,  Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga akizungumza na baadhi ya Watumishi  wa  Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na  kuwa Hifadhi za Taifa  wakati Naibu Waziri huyo  alipotembelea jana kwenye mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu  mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika  mapori hayo. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bihalamulo pamoja na baadhji ya watumishi wa TAWA na TANAPA wakati Naibu Waziri huyo  alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu  mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika  mapori hayo,  Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bihalamulo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga ( wa pili kushoto)  akioneshwa  eneo la Ziwa  Burigi katika eneo la Nkonje na Meneja wa  Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi kuwa Hifadhi za Taifa , Bigilamungu Kagoma  ( wa kwanza kushoto) wakati Naibu Waziri huyo  alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu  mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika  mapori hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga   akisaini kitabu cha wageni i katika eneo la Nyungwe  wakati Naibu Waziri huyo  alipotembelea jana mapori hayo katika ziara yake ya siku tatu  mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika  mapori hayo,  Watatu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bihalamulo, Sada Malunde
1.    Baadhi ya mafuvu ya wanayamapori katika Pori la A kiba la Burigi katika eneo la Nyungwe.
                    (Picha na Lusungu Helela -WMU)


Na. Lusungu Helela -Kagera.
Bodi ya Wadhamini ya Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) imeidhinisha na kuruhusu matumizi  ya bajeti ya mpito ya kiasi cha shilingi 3.9 bilioni zitumike kwa ajili ya  kuimarisha uhifadhi, uendelezaji utalii pamoja na ujenzi wa miundombinu katika Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa.

Hatua hiyo imekuja kufuatia tangazo la Serikali la kuyapandisha  hadhi Mapori ya Akiba ya Bihalamulo,Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa  kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamisi Kigwangalla wakati  alipokuwa akihitimisha  bajeti ya Wizara mwezi Mei  mwaka huu Bungeni mjini Dodoma.

Ofisa Mwenye Wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi, Damian Saru amesema hayo jana  mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga  wakati alipotembelea  mapori ya Biharamulo, Burigi na Kimisi ( BBK) ikiwa ni  ziara yake ya   kikazi ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua ya uendelezaji iliyofikiwa na TANAPA katika  mapori hayo.

Alitaja fedha hizo kuwa  zimeshaanza kutumika katika kuimarisha ulinzi, kujenga miundo mbinu ya utalii na Utawala, kuainisha mipaka , kusimamia mchakato wa kupandisha hadhi mapori

Damian Saru, Ofisa mwenye wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi aliyeteuliwa na TANAPA, aliwasilisha taarifa hiyo pamoja na kumweleleza Naibu Waziri huyo hatua za utekelezaji zilizofikiwa katika mapori hayo. 

Alimweleza kuwa askari 58 wameshafika kwenye mapori hayo matano kwa ajili ya kuongeza nguvu. Mashine ya kutengeneza barabara ' Motor Grader moja imeletwa kwa sjiki ya kutengeneza barabara.

Pia, Alimweleza Naibu Waziri huyo ikiwemo vitendea kazi ikiwemo ndege moja magari manne, mahema silaha, GPS vimeletwa katika mapori hayo kwa ajili ya kuimarisha utendaji kazi,Kufuatia utekelezaji huo, Mkuu mwenye hadhi ya Mkuu wa Hifadhi alitaja mafanikio yaliyopatikana katika kIpindi kifupi cha utekelezaji maagizo hayo kuwa katika kipindi cha wiki mbili pamoja na ng'ombe 41 kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Pia , Alitaja idadi ya watuhumiwa 12 wa ujangili wamekatwa. Aidha, Saru alitaja aina za vifaa vilivyokatwa kuwa ni mitumbwi mitatu, mkaa gunia mbili pamoja na baiskeli zopatazo 10.

Kwa upande wake, Naibu Waziri , Mhe.Hasunga ameridhishwa na hatua ya TANAPA kwa ushirikiano na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) kwa nzuri waliyoifanya.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.