Habari za Punde

Wananchi wa Zanzibar Waadhimisha Siku ya Unyonyeshaji Katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni.

 Naibu Waziri wa Afya Harusi Suleiman akizungumza na wananchi katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyshaji duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Abdalla akisisitiza  umuhimu wa akinamama kunyonysha watoto wao maziwa ya kifua ili wakuwe wakiwa na afya bora.
Mama Salha Hamis akiwa na mtoto wake Baidar Abdalla aliemnyonyesha maziwa ya kifua pekee katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo akitoa ushuhuda katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yaliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil.
 BAADHI ya wananchi walioshiriki kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya {hayupo pichani} katika kilelel cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji katika Ukumbi wa Saheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni.
MATEMBEZI ya Maadhimisho wiki ya Unyonyeshaji katika Ukumbi wa Shekhe Iddrisa Abduliwakili Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Na Ramadhani Ali – Maelezo.
Naibu Waziri wa Afya Harusi Suleiman amesema asilimia kubwa ya wazazi hawafuati taratibu zinazotakiwa katika kunyonyesha watoto wao na kupelekea watoto wengi kupata homa za mara kwa mara ikiwemo mtapiamlo.
Alisema asilimia 20 tu ya akinamama ndio wanaokidhi taratibu nzuri za kunyonyesha  maziwa ya kifua Zanzibar na asilimia iliyobaki wanafuata tamaduni za kigeni za kutumia maziwa ya kopo ambayo hayako salama kwa ukuaji wa watoto.
Naibu Waziri alieleza hayo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji duniani ambapo kwa Zanzibar yalifanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil Kikwajuni.
Alizitaja taratibu nzuri za kunyonyesha mtoto kuwa ni pamoja na mama kuwa na utulivu wakati wa kunyonyesha, kuanza kunyonyeshwa saa moja baada ya  kuzaliwa, mtoto kunyonya maziwa ya kifua pekee miezi sita ya mwanzo na kuendelea kunyonyeshwa hadi kumaliza miaka miwili.
Alisema kumyonyesha maziwa pekee mtoto katika kipindi cha miezi sita ya mwanzao bila kumpa chakula chengine, hata maji, kunapelekea kukua  akiwa na afya bora.
Aliongeza kuwa maziwa ya mama ni moja ya haki ya msingi ya mtoto na yanamlinda na maradhi mbali mbali yakiwemo ya kuharisha, kupungua uzito na huwaepusha na vifo kwasababu yanavirutubisho vyote muhimu kwa afya yake.
Hata hivyo alisema kazi ya kumlea mtoto inahitaji ushirikiano wa karibu wa familia na taasisi za Serikali na taasisi binafsi na ndio sababu mzazi akapewa miezi mitatu ya likjizo baada ya kujifungua na kuruhusiwa kuondoka kazini kabla ya wakati wa kawaida kwa ajili ya kwenda kumpa mtoto.   
Mkurugenzi wa Idara ya Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Abdalla alisema unyonyeshaji mzuri wa watoto ni moja ya chanzo cha kuwa na taifa lenye maendeleo kwani watoto watakua wakiwa na afya na kufanyakazi vizuri.
Aliwashauri wazazi kuwapa chakula kwa mpangilio mzuri watoto wanapotimia umri wa miaka miwili ili kuwaepusha na maradhi yasiyoambukiza ambayo yameongezeka sana hivi sasa na matibabu yake ni gharama kubwa.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mwakilishi wa Shirika la UNICEF  Said Juma Othman aliahidi kuwa mashirika ya Kimataifa yaliopo Zanzibar yataendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuhakikisha watoto wanapatiwa haki zao za msingi.
Ujumbe wa maadhimisho ya wiki  ya unyonyeshaji mwaka huu ni maziwa ya mama ni msingi bora wa maisha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.