Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Aendelea na Ziara Yake Wilayani Igunga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Igunga wakati alipoingia kwenye kiwanja cha Mnadani katika mji mdogo wa Igunga kuhutubia mkutano wa hadhara
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Singida,  Paskasi Mragili wakati aliposimama kwa muda mfupi miini Singida alipokuwa njiani kwenda Igunga mkoani Tabora kwa ziara ya kazi Agosti 16, 2018.  Mragili alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu  hadi Mamlaka hiyo ilipovunjwa. Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi wa Dini wakati alipowasili kwenye kiwanja cha Mnadani katika mji mdogo wa Igunga kuhutubia mkutano wa hadhara
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo.  
Wananchi wa Igunga wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika kiwanja cha Mnadani kwenye mji  mdogo wa Igunga, Agoisti 16, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.