Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Atembelea Kiwanda Cha Viuatilifu Cha Labiofam Kilichoko Kibaha.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama katika darubini uwezo wa dawa ya kuua viluilui vya mbu wakati alipotembelea kiwanda cha viuatilifu cha LABIOFAM kilichopo  Kibaha mkoani Pwani, Agosti 29, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo na wapili kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Mhandisi Aggrey Ndunguru
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama hatua za utengenezaji wa dawa ya kuua viluilui vya mbu wakati alipotembelea kwanda cha Viuatilfu cha LABIOFAM kilichopo Kibaha mkoani Pwani, Agosti 29, 2018.   Watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evaresti Ndikilo, wapili kushoto ni Menaja Uzalishaji wa kiwanda, Mhandisi  Aggrey Ndunguru na kushoto ni Mtalaam wa Biolojia wa kiwanda(micro biology), Jovin Magayane
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji wa kiwanda cha Viuatilifu cha LABIOFAM kilichopo  Kibaha Mkoani Pwani, Mhandisi  Aggrey Ndunguru (kushoto) wakati alipotembelea kiwanda hicho
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mtambo wa kutengeneza dawa ya kuua viluilui vya mbu wakati alipotembelea kiwanda cha viuatilifu cha  LABIOFAM kilichopo Kibaha mkoani Pwani, Agosti 29, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama madumu ya dawa ya kuua viluilui vya mbu wakati alipotembelea kiwanda cha Viuatilifu cha LABIOFAM kilichopo Kibaha mkoani Pwani
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vichupa vya dawa ya kuua viluilui vya mbu wakati alipotembelea kiwanda cha viuatilifu cha LABIOFAM kilichopo  Kibaha mkoani Pwani Agosti 29, 2018 . Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo, kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda, Mhandisi Aggrey Ndunguru na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Dkt. Samuel Nyantahe
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vichupa vya dawa ya kuua viluilui vya mbu wakati alipotembelea kiwanda cha viuatilifu cha LABIOFAM kilichopo  Kibaha mkoani Pwani, Agosti 29, 2018 . Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo, kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda, Mhandsi Aggrey Ndunguru.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  baada ya kutembelea kiwanda cha viuatilifu cha LABIOFAM kilichopo Kibaha mkoani Pwani,
Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kutembelea kiwanda cha viuatilifu cha LABIOFAM kilichopo Kibaha mkoani Pwani
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa kiwanda cha viuatilifu cha LABIOFAM kilichopo Kibaha mkoani Pwani baada ya kukitembelea kiwanda hicho, Agosti 29, 2018. Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijaga na kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  na Waziri wa Viwanda,  Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (watatu kulia) baada ya kutembelea kiwanda cha viuatilifu cha LABIOFAM kilichopo Kibaha mkoani Pwani, Agosti 29, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Dkt. Samuel Nyantahe.


Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mikoa yote nchini waendeleze kampeni ya kutokomeza ugonjwa malaria kwa kutumia dawa ya kuua viluilui vya mbu.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 29, 2018) alipofanya ziara katika kiwanda cha kutengeneza dawa ya kuua viluilui vya mbu kilichopo katika wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.

Amesema nchi inakabiliwa na matatizo makubwa ya ugojwa wa malaria, hivyo ni vema viongozi wa mikoa wakatokomeza viluilui vya mbu kwa kuwa dawa inatengenezwa nchini.

Waziri Mkuu amesema kiwanda hicho cha Labiofam ni cha pekee barani Afrika kwa kuwa na uwezo wa kutengeneza dawa za aina hiyo.”Tutumie fursa hii kutokomeza maralia nchini.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kutumia vyombo vya habari  kwa kuandaa vipindi vya kuelimisha umma kuhusu dawa wanayozitengeneza.

Amesema wananchi wanatakiwa kuelimishwa juu ya umuhimu wa kutumia dawa hiyo kwa ajili ya kuua viluilui katika maeneo ya makazi yao ili kuutokomeza ugonjwa wa maralia nchini.

Naye,Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Bw. Aggrey Ndunguru amesema dawa zinazotengenezwa kiwandani hapo zina uwezo wa kuua viluilui vya mbu tu na haina madhara kwa binadamu.

Amesemma dawa hiyo ambayo ipo katika ujazo tofauti tofauti inaweza kuwekwa kwenye makaro ya vyoo, maji yaliyotuama pamoja na katika matanki ya maji ili kuua viluilui.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu alifuatana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo na maafisa wengine wa Serikali.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.