Habari za Punde

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed Afanya Ziara ya Hafla Hospitali ya Mnazi Mmoja Kuangalia Changamoto Katika Hospitali Hiyo leo.

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akiskiliza changamoto mbali mbali za Wananchi waliofika Katika Hospitali kuu ya Mnazi Mmoja alipokua akifanya ziara ya kutembelea hospitali hiyo.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akiangalia vipande vya mahudhurio vya Wagonjwa wanaokuja kupata huduma ya Ultrasound.(Picha na Maryam Kidiko Habari Maelezo Zanzibar.)

Na.Khadija Khamis  na  Amina  Mkubwa. Maelezo  Zanzibar .
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed  amewasisitiza wananchi kuvitumia vituo vya afya vilivyo karibu nao kwa maradhi ya kawaida ili kuepusha msongamano katika  Hospitali  Kuu ya  Mnazi Mmoja.
Hayo ameyasema huko katika Hospitali ya Mnazi Mmoja wakati alipofanya ziara katika sehemu mbali mbali ambazo zinazotolewa huduma katika hospitali hiyo kutizama jinsi huduma zinavyotolewa kwa wagonjwa .
Alisema  hali ya  wagonjwa ni wengi jambo ambalo linawafanya madaktari na manesi kuzidiwa hivyo iko haja ya wagonjwa kuvitumia vituo vya afya vilivyo karibu ili kuepusha wingi wa wagonjwa hao .
Miongoni mwa sehemu ambazo alizotembelea ni chumba chaX–ray,Ultrasound,chumba cha wajawazito( Maternity),Sea view ENT Theatre Sehemu ya moyo  ( ECG ) pia na Jengo la kifua kikuu  ,Meno , Sehemu ya Sukari na Presha   Jikoni na sehemu nyenginezo za hospitali hiyo.
Aidha alisema kumejitokeza baadhi ya malalamiko kwa wagonjwa ambao imesemekana  kuwa kuna upendeleo mkubwa kwa baadhi ya sehemu za kutoa huduma hizo ikiwemo sehemu ya Ultrasound  kunauzwa vipande kwa wagonjwa kimoja elfu 20 na 50 jambo ambalo ni kosa kisheria .
Alifahamisha kuwa katika ziara hiyo ilikuwa na lengo la kufatilia taarifa hizo na imeonekeana wafanyakazi na 10 ambao wanahitaji  kusaidiwa kupata  huduma kwanza  na10 ni wagonjwa wa kawaida .
Pia alisema kuwa Serikali ina lengo la kutoa huduma  ya kuwapatia matibabu  wananchi wake hivyo wafanyakazi watumie utaratibu mzuri ili kuepusha manung’uniko kwa wananchi .
Hata hivyo alieleza hali ya jikoni katika hospitali hiyo si ya kuridhisha kutokana na uchafu uliopo  na kuwataka  wafanyakazi kubadilisha mazingira hayo mara moja ili kuhakikisha huduma za chakula ni bora kwa afya ya wagonjwa
 Vilevile alisema katika ziara hiyo imeonyesha  kuwa sehemu ya jengo ambalo inatolewa huduma ya kifua kikuu TB ya kawaida na kifua kikuu sugu haliridhishi  na ameahidi  atalishughulikia ili kufanyiwa matengenezo .
Alieleza kuwa bado zipo kasoro ndogo ndogo kwa wafanyakazi ambazo zinazojitokeza ikiwemo kuwatolea maneno yasiofaa kwa wagonjwa jambo ambalo ni kosa kwa mtumishi wa Serikali lakini kunashindikana kutolewa uwamuzi kwa sababu muhusika ambae anafanya kosa hilo hatajwi na mlalamikaji .
“tutashindwa kumuhukumu  mfanyakazi semeni nani kakutoleeni ukali muelezeni tumjue kwani maneno matupu tutakuwa na uhakika gani “alisema Waziri Hamadi.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI NA MAELEZO 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.