Habari za Punde

BARAZA LA NNE LA WAFANYAKAZI MOI LAFUNGULIWA, WAJIVUNIA UBORA

 Katibu mpya wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI, Bwana Ngina Mitti akibadilishana nyaraka na kupngezwa na aliyekuwa Katibu wa Baraza hilo Bwana Patrick Mvungi (kulia) baada ya kumaliza  muda wake wa miaka mitatu. Anayeshuhudia katikati ni Naibu Katibu mpya wa Baraza hilo Bi. Everlyne Machumu.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface (Kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi akimpongeza na kumkaribisha Katibu mpya wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI, Bwana Ngina Mitti baada ya kuchaguliwa kwenye Baraza hilo la Nne.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi akisoma hotuba ya ufunguzi wa Baraza hilo la Nne la Wafanyakazi wa MOI, Kushoto kwake ni Katibu mpya wa Baraza hilo Bwana Ngina Mitti na kulia ni Naibu Katibu wa Baraza Bi. Everlyne Maachumu.

Picha ya pamoja ya Baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya MOI wakati wa Baraza la nne lililofunguliwa rasmi leo Septemba 22 na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk Respicious Lwezimula Boniface katika ukumbi wa mikutano wa  IDDI NYUNDO, Halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Na.Andrew Chale -Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ajali na 
upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dk 
Respicious Lwezimula Boniface amefungua rasmi Baraza la 
Nne la Wafanyakazi katika ukumbi wa mikutano wa  IDDI 
NYUNDO, Halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Dkt. Respicious Boniface amefungua baraza hilo kwa 
kumwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini MOI, Bi. 
Zakia Meghji ambapo vikao hivyo vitafanyika kwa muda wa 
siku tatu  huku Wajumbe kutoka katika kila idara, vitengo na 
chama cha wafanyakazi wa MOI (TUGHE),Wajumbe wa 
TUGHE mkoa huku kwa upande wa Ofisi ya Waziri Mkuu-
Utumishi ikiwakilishwa na Bi.Tulia Msemwa.

Akizindua Baraza hilo Dkt. Boniface kwanza alitoa pole kwa 
tukio la ajali ya  kuzama kwa kivuko kilichotokea kwenye 
Ziwa Tanganyika cha MV Nyerere na kupoteza watu wengi 
huku pia ametoa pole kwa Rais na Watanzania wote.

Aidha akizungumza kwenye ufunguzi huo, Dk. Boniface 
amesema kuwa Taasisi hiyo imenufaika na mageuzi 
makubwa katika kipindi cha miaka mitatu kwa huduma 
zimeboreka  sana na zaidi ya Wagonjwa wa nje (Outpatient) 
zaidi ya Laki mbili wamehudumiwa katika kipindi cha 
mwaka wa fedha 2017/18.

“MOI ni ‘high Class Hospital, na huduma zetu ni bora sana 
ukilinganisha na Hospitali nyingine hapa Nchini na Nchi za 
Afrika Mashariki na Kati” Alisema Dkt. Boniface.

Dkt. Boniface amesema azma  ya Serikali ya awamu ya tano 
inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha 
Watanzania wote wanapata huduma zote  hapa  ambapo kwa 
hilo Nchi imefanikiwa sana.

“Kwa upande wa mifupa na ajali tuko vizuri na hakuna 
anayekwenda nje ya Nchi. Ila kwa upande wa upasuaji wa 
Ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kuna wachache 
wanakwenda  ila Serikali inaliangalia hilo na vifaa 
vimenunuliwa na hakuna atakayekwenda nje ya Nchi tena.

Fedha za kununulia vifaa zilitolewa na Serikali yetu sikivu 
kiasi cha Tsh. 16.5 Bilioni ambazo zimeiwezesha MOI kuwa 
na vifaa vya kisasa vya MRI, CT-SCAN, X-ray, Utra Sound, 
na vingine vya kazi muhimu kwa matatizo hayo hivyo Baraza 
hili liwe chachu ya kukuwa kwa taasisi yetu.” Alisema Dkt. 
Boniface.
Aidha, Dkt. Boniface ameongeza kuwa, kwa sasa wanataka 
kupunguza msongamano wa kwa wagonjwa wa 
nje wanaofika kupatiwa matibabu ya kliniki kwa kujenga 
jengo la kisasa huku pia mpango huo ni pamoja na 
kuanzisha mfumo maalum wa wagonjwa kufanya mihadi ya 
kuonana na Daktari kwa njia ya mtandao.

“Tunataka tuanzishe ‘propper data base’ ya uhakika yaani 
kila anayeingia anajulikana na anaonekana ili kuondoa ili 
suala la wagonjwa kuwahi namba hapa ambapo wanakuja 
kuanzia saa 12  alfajili hii sasa itakoma. Mfumo huu 
utasaidia sana hivyo kwa sasa tunajipanga kwa hilo na 
watalaam nimeshaongea nao” alimalizia Dkt. Boniface.

Katika hatua nyingine, Baraza hilo liliweza kupata Katibu 
mpya  Bwana  Ngina Mitti huku Msaidizi wake Bi. Evelyne 
Machumu baada ya aliyekuwa Katibu wa Baraza hilo Bwana 
Patrick Mvungi kumaliza  muda wake.

Baraza hilo la Wafanyakazi limehudhuliwa na wajumbe zaidi 
ya 70 huku pia pia wadau mbalimbali wakiwemo SSRA 
ambao walitoa mada juu ya kuunganishwa kwa mifuko ya 
hifadhi ya Jamii sambamba na Benki ya NMB ambao ni 
waadu wakubwa wa MOI ambao walitoa elimu na mafunzo 
namna ya benki hiyo inavyoweza kuwasaidia wateja wake 
wakiwemo wafanyakazi wa MOI.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.