Habari za Punde

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Aweso Amtaka Mkandarasi wa Mradi wa Maji Pangani Kumaliza Kwa Wakati Mradi Huo.NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani[CCM akizungumza katika mkutano wa hadhara eneo sokoni wilayani Pangani kabla ya kushuhudia utiliaji wa saini ya mkataba wa maji kutiliana saini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo baina ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga-Uwasa) wilayani hapo.
 MKUU wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah akizungumza katika mkutano huo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ni Katibu tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassan Nyange
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Hamisi Mnegero akizungumza katika mkutano huo

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga-Uwasa) Phares Aram kushoto akisaini  hati za mkataba wa maji na Mkandarasi a Mkurugenzi wa Kampuni ya Macarious Hotel and Co.Ltd Filbert Mmassy kulia ambaye atatekeleza mradi wa maji wilayani Pangani wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji kushoto na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katikati
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigel,a katika akiwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani  Zainabu Issa wakifuatilia mkutano huo kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Hamisi Mnegero akifuatiwa na Naibu WAziri wa Maji na Umwagiliaji ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Pangani CCM Jumaa Aweso
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amemtaka mkandarasi toka Kampuni ya Macarious Hotela and Co.Ltd ya Jijini Tanga kumaliza mradi wa maji katika mji wa Pangani wenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 500 kwa wakati kabla ili kuweza kutoa fursa kwa wananchi kunufaika na huduma hiyo muhimu.

Aweso ambae pia ni Mbunge wa Pangani ameyasema hayo wakati wa zoezi la kutiliana saini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo baina ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga-Uwasa) Wilayani hapo.

“kwa kweli hatuta kuwa na msamaha kwa Mkandarasi atakae kwenda kinyume na matakwa ya utekelezaji wa mradi huu kama yalivyoainishwa katika mkataba tutakuwa wakali kweli”Alisema Aweso.

Aidha alisema mradi huo utawanufaisha wananchi wa Pangani Mashariki na Magharibi ambapo unatarajiwa kutekelezwa ndani ya kipindi cha miezi kumi kama makubaliano yalivyoafikwiwa na pande mbili upande wa Serikali na Mkandarasi.

Alisema Wizara hiyo ya Maji na Umwagiliaji imetenga fedha hizo ili kutatua kero za wananchi wa maeneo hayo hivyo Serikali haitakuwa na uvumilivu na mkandarasi atakae kwamisha jitihada hizo za Serikali.

Hata hivyo amewataka viongozi wa Serikali na na mamlaka husika zilizopewa dhamana ya kusimamia mradi huo watambue wanao wajibu wa kuhakikisha wananchi wa maeneo hayo wanapata maji kama ilivyokusudiwa.

“Kumekuwepo na tabia ya uzembe kwa baadhi ya watendaji wetu kuwafumbia macho wakandarasi na kupelekea miradi mingi hapa nchini kutokukamilika kwa wakati wataalamu kuweni makini fedha hizi ni za walipa kodi si busara ziliwe hovyo”Alisema Aweso.

Nae Mkuu wa Mkoa Tanga aliyekuwa mgreni kushuhudia kutiliana saini mkataba huo alitoa tahadhari juu ya matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi hasa katika miradi inayoendelea kutekelezwa na kusema fedha hizo zitumike kwa lengo la wananchi.

“Labda nitoe tahadhari ya matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi huu si wakati wa kuchezea fedha hizi na lazima tuiwe makini na wakali pindi mmoja wetu anapobaini kwenda kinyume na matakwa yaliyoainishwa”Alisema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga-Uwasa) Faris Haram alisema jukumu la Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji katika Mji wa Pangani watahakikisha mradi huo unamalizika kwa wakati.

Haram alisema lengo kumuwezesha mwananchi wa maeneo hayo yaliokusudiwa anapata maji kama matakwa ya mradi yanavyoelekeza jambo ambalo linaweza kupunguza kero hiyo ya miaka mingi kama si kumaliza kabisa.

“Sisi kama viongozi wa Mamlaka hizi nza maji toka ngazi ya Mkoa na Wilaya tuliopewa dhama ya kusimamia mradi tutahakiksha wananchi hawa nawapata maji safi na salama tena kwa wakati”Alisema Aram.

Awali akisoma taarisa fupi mbele ya Naibu Waziri huyo Meneja wa Mamlaka ya Maji katika Mji wa Pangani(P-uwasa)Adam Sadiki alisema mradi huo utahusisha utafiti wa maji chini ya ardhi na kuchimba kisima kirefu kimoja.

Aidha alisema mbali na hilo pia utahusisha ukarabati wa visima vine kijijini boza,upanuzi wa miundombinu ya maji kwa kulaza mabomba yenye vipenyo tofauti na ufungwaji wa pampu mpya ya kusukuma maji katika Kijiji cha Mwembeni na ununuzi wa dira 600.

Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya Macarious Hotela and Co.Ltd Filbert Mmassy inayotekeleza mradi huo amewatoa shaka wananchi wa maeneo hayo kwa kusema yupo tayari kuanza rasmi mradi huo na matarajio yake kumaliza ndani ya miezi sita badala ya miezi kumi kama makubaliano yalivyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.