Habari za Punde

Kampuni ya Zanlink Liquid Telecom Yawadhamini Wacheza Golf Watatu Kushiriki Michuano ya Rotary Zanzibar &Fumba Town Golf Day Yatakayofanyika Katika Viwanja Vya Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar kesho.29/9/2018.


Mwakilishi wa Taasisi ya Rotary Zanzibar &Fumba Town Golf Day Bi. Sjani Miiggenburg, akimkabidhi Tiketi ya kushiriki michuano ya Golf ya Kimataifa yatakayofanyika katika Viwanja vya Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar, Mchezaji wa Timu ya Kikwajuni Golf Issa Mohammed Chapchap, katikati Afisa Masoko na Manunuzi wa Kampuni ya Zanlink Kelvin Leonard Kampuni ya Zanlink Liquid Telecom imewadhamini Wachezaji watatu wa mchezo huo kutoka Timu ya Kikwajuni.hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa kampuni hiyo majestic Zanzibar.    
Mchezaji wa Timu ya Golf ya Kikwajuni Mussa Foum akipokea Tiketi ya kushiriki michuano ya Kimataifa ya mchezo huo yajulikanayo kwa jina la Rotary Zanzibar &Fumba Town Golf Day, yatakayofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Kitalii Sea Cliff Zanzibar.katikati Afisa Masoko na Manunuzi wa Kampuni ya Zanlink  Liquid Telecom Ndg Kelvin Leonard, akishuhudia makabidhiano hayo yaliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo Majestic Zanzibar.
Mchezaji wa Timu ya Golf ya Kikwajuni Kassim Tall, akipokea Tiketi ya kushiriki michuano ya Kimataifa ya mchezo huo yajulikanayo kwa jina la Rotary Zanzibar &Fumba Town Golf Day, yatakayofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Kitalii Sea Cliff Zanzibar.katikati Afisa Masoko na Manunuzi wa Kampuni ya Zanlink  Liquid Telecom Ndg Kelvin Leonard, akishuhudia makabidhiano hayo yaliofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo Majestic Zanzibar.
Afisa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zanlink Liquid Telecom Ndh Kelvin Leonard akimkabidhi fulana Mchezaji wa Golf Zanzibar ni mmoja wa mshiriki wa michuano hiyo Ndg. Issa Mohammed Chapchap, Zanlink imewadhamini wacheza hao Watatu wa Golf Zanzibar kuweza kushiriki kwa mara ya pili katika mchezo huo unaofanyika katika Hoteli ya Kitalii ya Sea Cliff Zanzibar. 


Afisa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zanzlink Liquid Telecom Zanzibar Ndg. Kelvin Leonard akizungumza wakati wa mkutano huo na kutowa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusiana na kuwadhamini Wachezaji watatu kushiriki katika michuano hiyo ya Golf ya Kimataifa yanayofanyika kwa mara ya Pili katika Hoteli ya Kitalii ya Sea Cliff Zanzibar na kuwashirikisha Wachezaji wa Kimataifa 52 watashiriki michuano hiyo yanayofanyika kesho katika viwanja hivyo. 
Washiriki wa michuano ya Mchezo wa Golf Zanzibar wakifuatilia mkutano huo wa kutowa taarifa kwa waandishi wa habari kukamilika kwa michuano hiyo inafanyika Zanzibar katika Hoteli ya Kitalii kwa mara ya Pili katika viwanja vya Hoteli ya Sea Cliff Zanzibar. 
Mwandishi wa Kituo cha Tv Online cha KTV Zanzibar akiuliza suali wakati wa mkutano huio wa kutowa taarifa ya kukamilika kwa michuano ya Kimataifa ya Golf yatakayofanyika kesho katika viwanja vya Hoteli ya Kitalii ya Sea Cliff Zanzibar na kushirikisha Wachezaji wa kimataifa wa mchezo huo Afrika.na Nje ya Afrika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.