Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Naibu Waziri Mkuu wa China Mr. Han Zheing.


Jamuhuri ya Watu wa China itaendelea kuzingatia nafasi ya Tanzania katika kudumisha  uhusiano wake wa Kiuchumi, Maendeleo na Ustawi wa Kijamii kutokana na ushirikiano wa pande hizo mbili ulilolenga kusaidia Nchi changa katika Mpango wake wa Kushirikiana kwa karibu zaidi na Mataifa ya Bara la Afrika.
Naibu Waziri Mkuu wa China Bwana Han Zheing alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Ujumbe wake hapo katika Makaazi ya Wageni mashururi wa Kimataifa  Villa 7 Mjini Nanning Jimbo la Guangxi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.