Habari za Punde

Mchezo wa Kombe la Ujamaa Sports Club Kati ya Malindi na Mchangani United Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Malindi Imeshinda Bao 2-0.

Mshambuliaji wa Timu ya Malindi Khamis Rais akimpita beki wa Timu ya Mchangani United Salum Ali wakati wa mchezo wao wa Kombe la Bonaza la Timu ya Ujamaa Spotrs Club kuadhimisha miaka 61 tangu kuazishwa Timu hiyo ilioazishwa miaka 1957, Katika mchezo huo Timu ya Malindi imeshinda bao 2-0.
Mshambuliaji wa Timu ya Malindi kushoto Mohammed Mussa akimpita beki wa Timu ya Mchangani Salum Ali, wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Kombe la Timu ya Ujamaa Sports Club kuadhimisha miaka 61 tangu kuazishwa kwa timu hiyo Mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Malindi imeshinda mchezo huo bao 2-0.

Timu ya Malindi imeungano na Timu za Rastazoni, Taifa ya Jangombe katika mchezo wa Robo Fainali ya Michuano ya Bonaza la Tamasha la Maadhimisho ya Miaka 61 ya Timu ya Ujamaa Spotrs Club kutimiza miaka 61 tangu kuazishwa kwake mwaka 1957.

Timu ya Malindi imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali baada ya kuifunga Timu ya Mchangani United kwa bao 2-0. mchezo uliofanyika Uwanja Amaan Zanzibar Timu ya Malindi imeonesha mchezo mzuri katika mchezo wake huo na kuweza kusonga mbele katika michuano huo na kufikia hatua ya robo fainali. 

Malindi wameandika bao lake la kuwanza kupitia mshambuliaji wake Mohammed Said katika dakika ya 35 ya mchezo huo kipindi cha kwanza, Vijana wa Timu ya Mchangani wameweza kuonesha kiwango kizuri wakati wa mchezo huo lakini bahati haijawa yao kutokana na washambuliaji wake kukosa nafisi nyingi. hadi mapumziko Timu ya Malindi ikiongoza kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kiliaza kwa mashambulizi katika lango la Timu ya Malindi lakini mashulizi hayo hayajaleta matunda kwa kutomi huyo, Malindi wameandika bao lake la pili kupitia mshambuliaji wake Mohammed Said (Messi) katika dakika ya 85 ya mchezo huo kipindi cha pili, hadi mwisho wa mchezo huo Timu ya Malindi imetoka kifua mbele kwa bao 2-0. 
Michuano hiyo inaendelea leo kwa mchezo wa mwisho wamakundi Kati ya Mlandege na Muembeladu utakaofanyika saa kumi jioni Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mshambuliaji wa Timu ya Malindi Mohammed Mussa akimpita beki wa Timu ya Mchangani Salum Ali wakati wa mchezo wa Kombe la Ujamaa Sports Club uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar Timu ya Malindi imeshinda bao 2-0.Mshambuliaji wa Timu ya Malindi Mohammed Said Messi akiipatika timu yake ya Malindi bao la kwanza katika dakika ya 35 ya mchezo huo kipindi cha kwanza. 
Benchi la ufundi la Timu ya Mchangani United wakiwa na majozi baada ya Timu yao kukubali kipigo cha bao 2-0, dhidi ya Timu ya Malindi katika mchezo wa michuano ya Kombe la Bonaza la Timu ya Ujamaa Sports Club mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar.Viongozi wa Wachezaji wa Timu ya Malindi wakifuatilia mchezo wao na Timu ya Mchangani United wakati wa mchezo wao wa Kombe la Bonaza la Timu ya Ujamaa Sports Club kuadhimisha Miaka 61 ya Kuazishwa kwa Timu hiyo mwaka 1957 Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.