Habari za Punde

Mkutano wa Wazi wa Kupokea Maoni ya Wananchi Kuhusiana na Vitendo Vya Udhalilishaji Zanzibar Viwanja Vya Watoto Kariakoo Zanzibar.

Mwenyekiti wa Mkutano wa Wazi wa Kupokea Maoni ya Wananchi Dhidi ya Mapambano ya Ukatili na Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Jaji Mshibe Ali Bakari akiongoza mkutano huo katika viwanja vya ukumbi wa Kiwanja cha Wawtoto Kariakoo Zanzibar kulia Naibu Waziri wa Kaji Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Shadya Mohammed na kushoto Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe. Maudline Cyrus Castico, wakifuatilia michango ya Wananchi waliohudhuria mkutano huo leo. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Masuala ya Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto Zanzibar Bi. Chiku Marzuku akichangia mkutano huo akitowa maonu yake kuhusiana na kukithiri kwa vitendo hivyo vya udhalilishaji Zanzibar na kutowa rai ya chukukuliwa kuweza kuzuiya vitendo hivyo kwa Serikali kupitia Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar walioanda mkutano huo wa kupokea maoni ya wananchi.
Mwananchi Abdul Mshangama akichangia wakati wa mkutano huo wa wazi kutowa maoni jinsi ya mapambano ya Ukatili na Udhalilishaji wa Wanawake na Watoto, na kuchangia kwa kiasi kikubwa Wazazi huchangia vitende hivyo kwa kuwaachia Watoto wao muda mungi wakiwa nje hadi usiku mkubwa na kushauri kuchukuliwa hatua za kisheria kuwekwa kwa muda maalum kwa Watoto kuwa nje usindizi saa moja usiku na wakikutikana wawezi kupikwa mikwaji kwa kupatikana makosa ya kuwa nje muda huo.Na kutoa mifano katika miaka ya sabini na thamani alikuweke Mzee maarufu kwa jina la sakabona watoto wengi kipingi hicho walikuwa wakimuongopa na kutokwa nje zaidi ya saa moja usiku. 
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Wilaya ya Mjini Unguja Ndg.Bilal Said akichangia na kutowa maone yake wakati wa mkutano huo akichangia na kusema Vijana hawakushirikishwa katika sheria mbalimbali na hawamu katika sheria zao ya Wanawake ndio pekee wao katika sheria hizo. ameitaka taasisi husiku kuwashirikisha vijana ili kupunguza vitendo hivyo vya udhalilishaji.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.