STATE HOUSE
ZANZIBAR
OFFICE OF THE
PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 27.09.2018

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amemtumia salamu za pongezi Rais
wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping kwa kutimiza miaka 69 tokea
kuundwa kwa Taifa hilo.
Dk. Shein, alieleza kuwa
kwa niaba yake binafsi pamoja na wananchi wote wa Zanzibar wanatoa pongezi kwa
Rais Xi, wananchi wa China pamoja na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa
kutimiza umri huo wa Taifa hilo tokea kuasisiwa kwake.
Salamu hizo zilieleza kuwa Watu
wa Zanzibar wanapata faraja na matumaini kutokana na maendeleo makubwa
yanayoendelea kupatikana katika Taifa hilo la China kwenye sekta mbali
mbali za maendeleo na uchumi.
Aidha, salamu hizo zilieleza
kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi wake wataendelea
kutoa ushirikiano sambamba na kuimarisha uhusiano mkubwa uliopo kati yao na
ndugu zao wa China.
Pamoja na hayo, salamu hizo za pongezi
zilimtakia afya njema na mafanikio ya muda mrefu Rais wa Jamhuri ya Watu wa
China Xi Jimping katika kuliongoza Taifa hilo.
Uhuru wa Taifa hilo ulitangazwa
mnamo Oktoba 1, 1949.
Rajab Mkasaba,
Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024
2231822
E-mail:
rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment