Habari za Punde

Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd, Yachangia Kambi ya Wanafunzi wa Kidatu Cha Nne Wilaya ya Kaskazini B Unguja, Wakijiandaa na Mitihani Yao.

Afisa Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd Mohammed Khamis , akimkabidhi msaada wa Chakula Mchele Tani Moja Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja Mhe Rajab Ali Rajab, kwa Ajili ya Wanafunzi wa Skuli za Sekondari za Wilaya ya Kaskazini B Unguja wanaokaa kambi kujiandaa na Mitihani yao ya Kidatu cha Nne  mwaka huu 2018, ili kujiandaa kuweza kufanya vizuri mitihani yao na kufaulu kuendelea na masomo yao Kidatu cha Tano na Sita, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Faya Kilimani Zanzibar. 
Afisa Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd Chaguo la Watu Ndg Mohammed Khamis akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na msaada huo wa chakula tani moja ya mchele kusaidia Kambi wa Wanafunzi wa Kidatu cha Nne Wilaya ya Kaskazini B Unguja ili kutowa nafasi kwa wanafunzi hao kuweza kuweka kambi kujisomea na kufanya vizuri masomo yao katika mitihani ya Taifa 2018.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.